MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe aihamasisha Watanzania kuwa na desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kulinda miili yao na magonjwa nyemelezi mbalimbali.
Gondwe aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipomwakilisha Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima kwenye uzinduzi wa kituo cha mazoezitiba cha Kisiwani Clinic Centre (KCC) kinachojihusisha kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kulinda miili yao na magonjwa yanayoepukika.
Akijibu risala ya kituo hicho chenye lengo la kuipunguzia gharama Serikali kwa kuagiza madawa kwa gharama kubwa ili kuwafanya Watanzania kuwa salama, alisema kuanzia leo Wanachama wote wa KCC mtakuwa mabalozi sasa wakuhamasisha jamii ya Watanzania kufanya mazoezi kwani kazi mnayoifanya ni kubwa na mnaisaidia Serikali kwa kiasi kikubwa sana.
Mkuu wa Wilaya alisisitza kuwa yeye yuko tayari muda wote kuanzia sasa KCC ipeleke mapendekezo ni namna gani sasa wataifikia jamii yote kuhakikisha wanafanya mazoezitiba kwa faida ya kila mmoja nay eye atalisimamia hilo.
Nae Mbunge wa Jimbo la Kinondoni alimshukuru sana Mgeni Rasmi kwa kuacha ,majukumu yake kuungana na Wanajimbo lake kwa nia nzuri ya kuifanya Kinondoni kuwa Salama kwa kuihamasisha kufanya mazozi.
Tarimba aliwapongeza sana KCC na kuwaomba hamasa walioianzisha isiishie Kisiwani bali Jimbo zima la Kinondoni.Alisisitiza kwa staili hii mliyokuja nayo KCC naamini Jimbo langu sasa litahamasika kufanya mazoezi na kila mwanakinondoni atakuwa afya nzuri na salama.
Nae Mratibu na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi aliwashukuru Viongozi wote waliojitokeza kushiriki uzinduzi huo na kuwaomba ushirikiano siku nyingine wakiwahitaji kwa maana ya kuhamasisha jamii.
Uzinduzi huo uliambatana na huduma ya matibabu bure kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa manispaa ya Kinondoni ya kuchanja Uviko 19, kupima virusi vya ukimwi, kuchangia damu, kupima uzito, kupima saratani ya kizazi kwa Wakina Mama, Huduma ya Macho, huduma ya kinywa pamoja na elimu ya Bima ya Afya na Lishe Bora.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe( kwa niaba ya Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima) akionyesha moja ya Tuzo maalumu zilizotolewa kukabidhiwa wakati wa uzinduzi wa kituo cha mazoezi tiba cha Kisiwani Clinic Centre(KCC) ikiwa moja ni ya Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi kwa kuhamasisha jamii kufanya mazoezi nay a pili ni ya Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan kwa kupigania afya za Watanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Abbas Tarimba wakiwa na baadhi ya wanachama wa kituo cha mazoezitiba “Kisiwani Clinic Centre”(KCC) wakipasha viungo vya mwili ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mazoezitiba ya kituo hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam.Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya alimuwakilisha Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo cha mazoezitiba, Anuary Akrama na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Abbas Trimba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...