Katika
robo ya tatu ya mwaka iliyoishia Septemba 2021, Benki ya NMB imeonesha
ufanisi mkubwa na mafanikio katika maeneo mbalimbali ya kimkakati.
Kasi
ya ongezeko la mapato iliendelea huku uwekezaji katika maeneo mapya na
utekelezaji mipango endelevu ya kidijitali nayo ikiimarishwa pia.
Nidhamu
ya kukabiliana na hatari za kiuendeshaji na ya maswala yote ya utawala
bora yalizingatiwa kikamilifu kipindi chote cha robo hii ya mwaka.
Matokeo
ya kuimarika kiutendaji yameiwezesha NMB kupata faida kabla ya kodi ya
shilingi bilioni 302 na faida baada ya kodi ya shilingi Bilioni 211,
hili ni ongezeko la asilimia 43 ya faida iliyopatikana kipindi kama
hicho mwaka jana na zaidi ya faida ya kihistoria ya mwaka wote wa 2020
ambayo ilikuwa ni kiasi cha Shilingi bilioni 206.
Nidhamu ya hali
ya juu ya NMB katika kutekeleza mipango yake ya kimkakati imeendelea
kuiongezea imani kwa wateja na hivyo na kuifanya iimarike zaidi kwenye
nafasi yake ya benki inayoongoza nchini.
Katika kipindi cha miezi
9 kufikia mwezi Septemba 2021, jumla ya mapato ya NMB yalikuwa ni
Shilingi bilioni 721, kiasi ambacho ni asilimia 20 zaidi ya TZS bilioni
601 zilizopatikana kipindi kama hicho Mwaka 2020 ikichangiwa zaidi na
kuongezeka kwa mikopo na miamala.
Mikakati ya benki ya kudhibiti
gharama za uendeshaji imeendelea kuzaa matunda na kusababisha kuboreka
kwa uwiano wa matumizi na mapato halisi kufikia asilimia 47 kutoka
asilimia 52, kiwango kilicho ndani ya matakwa ya Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) cha asilimia 55. Benki inaendelea kuboresha utendajikazi na
uwekezaji hasa kwenye maeneo ya kimkakati.
Ubora wa mikopo
umeendelea kuimarika ambapo uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi
asilimia 3.8 kwenye robo ya tatu, kutoka asilimia 6.6 kipindi kama hiki
mwaka jana ikionyesha hatua nzuri iliyopigwa kudhibiti ukopeshaji
usiokuwa na tija.
NMB imeendelea kuwa na mizania madhubuti ambayo
ukuaji wake unaonyesha kuimarika kwa mahusiano na wateja wetu. Mwishoni
mwa robo ya tatu ya mwaka, mikopo iliongezeka kwa asilimia 13 hadi
kufikia shilingi trilioni 4.5 kutokana na kukua kwa mikopo kwenye maeneo
muhimu hasa kilimo, biashara ndogo na za kati pamoja na mikopo
binafsi.
Amana za wateja nazo ziliongezeka kwa asilimia 18 mpaka
shilingi trilioni 6.1 kufikia tarehe 30 Septemba 2021 ukilinganisha na
shilingi trilioni 5.3 mwezi Septemba 2020 kutokana na NMB kuendelea
kutoa suluhisho stahiki katika kuimarisha urahisi na upatikanaji wa
huduma za kibenki kwa wateja.
Mali zote za benki zilikuwa na
thamani ya shilingi trilioni 8.2 mwishoni mwa Septemba 2021, ongezeko la
asimilia 17 (YoY) kutoka TZS trilioni 7 kipindi kama hicho mwaka jana.
Akitoa
maoni yake juu ya utendaji huo na nafasi ya NMB sokoni, Afisa Mtendaji
Mkuu, Bi Ruth Zaipuna, alisema: “Timu ya wafanyakazi wetu imekuwa na
kipindi kingine chenye mafanikio kwa kuongeza faida ya miezi 9 kwa
asilimia 43, hali inayoonyesha kuendelea kuimarika kwa mazingira ya
kiuchumi na hatua madhubuti za sera za fedha zilizopitishwa na Benki Kuu
ya Tanzania.”
“Mkakati wetu wa uendeshaji umeendelea kuwa sahihi
huku mafanikio ya kuendeleza umiliki wa soko ukipelekea kupatikana kwa
faida kubwa.Tunaendelea bila kuchoka kuzingitia matakwa ya wateja na
tumeshuhudia kukua kwa kasi ya ukopeshaji na amana za wateja kwa mwaka
huu mzima,” Bi Zaipuna aliongeza.
“Tukiwa kinara wa Ajenda ya
maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi yetu, katika kipindi cha miezi
9 cha mwaka 2021 tumekuwa na mafaniko makubwa yafuatayo:
Tulitekeleza
mipango kadhaa kwenye uwekezaji katika shughuli za kijamii sanjari na
nguzo kuu za mikakati yetu. Upande wa afya tuliwafikia watu zaidi ya
elfu 48 (48,000) kupitia misaada ya vifaa tiba. Wanafunzi zaidi ya elfu
kumi (10,000) walinufaika na madawati tuliyoyatoa. Pia tuliwawezesha
vijana na watu wazima 3,500 kupata elimu hitajika katika maswala ya
fedha kupitia program yetu ya elimu ya kifedha kwa jamii
Tulifanikisha
mbio za NMB Marathon maarufu kama ‘‘Mwendo wa Upendo’’ zilizotuwezesha
kukusanya shilingi milioni 400 kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa
Fistula kwa akina mama.
Pia
hivi karibuni tumezindia mfumo wa ‘’sandbox environment’’unaozipa
kampuni chipukizi fursa ya kubuni suluhishi za kidijitali na kuzifanyia
majaribio kwenye mifumo yetu kwa minajili ya kujenga jamii ya
Kitanzania iliyojumuishwa kwa teknolojia za kisasa. .
Aidha, Bi
Zaipuna aliongeza kusema: “Tuna furaha na fahari kwamba mafanikio yetu
katika maeneo muhimu ya utendaji, ubunifu na huduma kwa wateja,
zietufanya tuweze kupata tuzo saba za kimataifa, zote zikiitaja NMB kuwa
benki bora Tanzania. Tuzo hizi zinaipa benki msukumo wa kuendelea kutoa
huduma bora zaidi sokoni.
“Tunawashukuru wateja wetu wenye
thamani kubwa kwetu, wanahisa, wadau wote na wafanyazi kwa ujumla kwa
kuendelea kutuunga mkono. Tunapoelekea kumaliza mwaka wa 2021 tuna
matumaini makubwa na safari iliyo mbele yetu na tutaendelea kujitolea
kusizadia jamii zote tunazozihudumia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...