Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Mpira wa Miguu kwa wanawake (Twiga Stars) kwa kutwaa kombe la COSAFA jana Oktoba 9, 2021 baada ya kuifunga timu ya Malawi.
 
Mhe Rais ameyasema hayo leo Oktoba 10, 2021 jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo Kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO -19. Akisoma  hotuba yake wakati alipokuwa akianisha  mafanikio ya Serikali yake  katika kipindi cha miezi sita ambapo kwenye eneo la Sanaa na Michezo amesifu kazi nzuri inayofanyika katika kipindi hiki.

 "Kipekee niwapongeze Twiga kwa kuchukua Kombe la COSAFA, na mara nyingi huwa nasema watoto wetu wa kike wanajitahidi sana. Hili ni kombe lao la tano nadhani kuleta nchini hivyo ninawaahidi kuwatambua” amefafanua Mhe. Rais.

Aidha amesema timu ya Taifa ya Soka  ya Vijana  chini ya miaka 23 ni miongoni mwa wanamichezo walioiwakilisha vema nchi yetu ambapo pia amewataja mabondia  Hassan Mwakinyo na Zulfa Macho kuwa wameipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa.

 Mhe. Rais amewapongeza pia wasanii sita waliofuzu shindano la Afrika la urembo, utanashati na mitindo kwa watu wenye usikivu hafifu watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano  hayo kidunia nchini Brazili Aprili mwakani.


Wasanii hao ni Khadija Kanyama, Carloyne Mwakasaka, Surath Mwanis, Russo Songoro, Rajani Ally na Joyce Denis

Pia amewapongeza na wasanii wengine 6 walioingia  kwenye mashindano ya AFRIMA ya wasanii nchini Marekani.
Amewataja wasanii hao kuwa ni Diamond, Ali Kiba, Mario, Nandy, Zuchu na Rosa Ree ambapo amewasihi watanzania wote  kuwatia moyo na  kuwaunga mkono hususan kuwapigia kura kwa wingi ili waibuke washindi katika shindano hilo.
 
Mhe. Rais amesisitiza kuwa  Sekta ya sanaa na michezo ni miongoni mwa sekta  muhimu hapa nchini zinazokuwa  kwa kasi na kutoa mchango mkubwa  katika uchumi na ajira ambapo amesema kwa kutambua hilo Serikali imeanzisha Mfuko  wa Maendeleo ya Sanaa ambao umetengewa kiasi cha shilingi 1.5 bilioni ambazo pia zitasaidia Timu za Taifa.

Kwa upande mwingine  amesema Serikali imetenga  Bajeti COSOTA kwa ajili ya kukusanya mapato ya wasanii  na kwamba ifikapo mwezi Desemba mwaka huu Wasanii wataanza kulipwa  mirabaha kwa ajili ya kazi zao wanazozifanya.
 
Akifafanua amesema Serikali imefuta kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye nyasi bandia ambapo pia amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Serikali kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo imeanzisha Tamasha Maalum la Michezo kwa  Wanawake (Tanzanite) na kuratibu Tamasha la Afrika la  urembo, utanashati na mitindo kwa watu wenye  ulemavu wa kusikia.  Pia kuanzisha tuzo za wasanii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Back To Top