SHIRIKA La Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Wizara ya Uvuvi na Mifugo na NBS wanashirikiana kuendesha zoezi la Sensa ya Vyombo Vidogo vya Usafiri Majini Jijini Mwanza na Tanzania Bara katika mialo mbalimbali.
Kabla ya kuendesha mazoezi hili yalitolewa mafunzo ya ukusanyaji wa takwimu za Sensa ya Vyombo vya Usafiri Majini na Uvuvi Tanzania Bara yaliyohusisha watendaji wa TASAC, NBS na Maafisa Uvuvi kutoka mikoa mbalimbali.
Lengo kuu la Sensa hii ni kutaka kujua idadi ya vyombo vidogo vya Usafiri Majini ili kutengeneza kanzidata itakayosaidia katika kupanga maendeleo ya kiusalama na kiuchumi katika Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...