Kampuni kongwe ya ulinzi nchini ya SGA imepongezwa kwa juhudi zake kubwa ambazo zimekuwa za msaada mkubwa kwa jeshi la polisi nchini katika kutekeleza majukumu yake.
Pongezi hizo zimetolewa na kamanda wa polisi wilaya ya Kinondoni SSP Ally Kwendo, Oktoba 1, 2021, wakati wa uzinduzi rasmi wa ushrikiano kati ya Jeshi la Polisi na kampuni ya SGA uliofanyika hivi karibuni.

Alisema SGA imekuwa na inaendelea kutoa ushirikiano wake huo maeneo yote nchini kupitia dhana ya ulinzi shirikishi kupitia polisi jamii,  ambapo alitoa wito kwa makampuni mengine ya kibinafsi ya ulinzi kuiga kazi nzuri zinazofanywa na kampuni ya SGA. Polisi jamii ni dhana ya kushirikisha jamii kwa lengo la kuhakikisha amani na usalama unakuweko katika maeneo yote nchini.

"SGA imekuwa washirika wakubwa wa Jeshi la Polisi Tanzania hata kabla ya wazo la polisi jamii halijaanzishwa hapa nchini na wamekuwa wakitoa ushirikiano wao nchini kote”, alisema SSP Wendo.

Aliongeza kwa kusema kuwa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi yako mbele katika kutekeleza majukumu ambapo alisema wafanyakazi wa makampuni hayo wako mstari wa mbele kila mara katika kuzuia uhalifu huku wakihakikisha usalama unakuwekmo maeneo wanayotoa huduma zao.

"Jeshi la polisi tunakusudia kuwajengea uwezo walinzi wa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi ili waweze kushiriki vyema katika kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao ya kazi”, alisema.

Aidha kamanda Wendo alichukua fursa hiyo kutoa salamu za pole kutoka jeshi la polisi kwa askari wa kampuni ya SGA aliepoteza maisha wakati wa tukio shambulio lililotokea Agosti 25, mwaka huu, maeneo ya ofisi ya Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Alisema Jeshi la Polisi lilimchukulia afisa huyo kama sehemu ya jeshi hilo na ndiyo sababu akapewa heshima zote anazostahili kupewa ofisa wa jeshi la polisi anapopoteza maisha akiwa kazini na kwamba askari huyo alikuwa ni kielelezo cha kujituma kunakofanywa na wafanyakazi wa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi katika kuhakikisha usalama unakuweko ndani ya jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SGA Tanzania, Bw. Eric Sambu, amesema kampuni hiyo inaadhimisha miaka 37 ya kufanya kazi nchini Tanzania, ambapo alisema katika kipindi hicho imepata mafanikio makubwa.

“Mafanikio haya yamekuwa makubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kutokana na mabadiliko ambayo uongozi wa kampuni yetu umefanya, sambamba na ushirikiano ambao tumekuwa tuliupata kutoka kwa wadau mbalimbali likiwemo jeshi la Polisi”, alisema na kuongeza uimarishaji wa wafanyakazi wa kampuni huyo umewawezesha wafanyakazi wake kufanya kazi na kukidhi ya wateja wao kampuni hiyo.

Aliendelea kusema kuwa mafanikio mengine ya kampuni hiyo pia yametokana na kuwa na wafanyikazi waaminifu, waadilifu na wenyebidii katika kutekeleza majukumu yao.
"Matukio ya hivi karibuni tukiyatafsiri katika mazingira ya kibiashara yametupatia fursa ya kujifunza sambamba na kutupa nafasi ya kuwajengea uwezo wafanyikazi wetu ili waweze kutekeleza majukumu yao na kukidhi mahitaji ya wateja wetu.

"Tunaendelea kurekebisha utendaji wetu wa kazi kwa kuwekeza katika teknolojia na wafanyakazi wenye weledi na waadilifu ili kuboresha huduma zetu”, alisema.
Kampuni ya ulinzi ya SGA wiki iliyopita ilishinda tuzo ya juu wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Madini ya Geita ya wiki iliyopita.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SGA Tanzania, Bw. Eric Sambu, pia yumo katika orodha ya Watendaji bora 100 hapa nchini Tanzania, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa 16 na atapewa tuzo yake yenye kuakisi sifa hiyo wiki ijayo.

SGA pia ilipigiwa kura na kuchaguliwa kama mtoaji wa huduma za ulinzi bora yenye vifaa na vya kuaminika zaidi wakati wa tamasha la tuzo hizo la mwaka wa 2020. Kampuni hiyo pia imafanikiwa kupata vyeti vingine tatu vya ubora katika nyanja za usimamizi wa Ubora (ISO 9001: 2015), Afya na Usalama Kazini (ISO 45001: 2018) na Mfumo wa Usimamizi wa Uendeshaji wa Usalama (ISO 18788: 2015).

SGA Ilianza kufanya shughuli zake jhapa nchini mnamo mwaka wa 1984, wakati huo ikijulikana kama Group Four Security (T) Ltd. SGA ni kampuni kongwe ya ulinzi ya kibinafsi hapa nchini Tanzania, ambapo kwa sasa inatoa ajira kwa Watanzania zaidi 6,000 walioko kwenye mtandao wa kampuni hiyo ulioko nchini kote.
Kampuni hiyo inatekelezaji majukumu yake yakiwa ni pamoja na ulinzi wa watu na maeneo yao, ulinzi kwa njia za kielektroniki, huduma za kukabiliana na dharura, pamoja usafirishaji wa fedha kwa njia za usalama.

"Tukiwa na magari 284 na vituo 12 vya kikanda, pamoja na vyumba vya mawasiliano vya uhakika vyenye watendaji waliobobea, ni wazi kuwa tuna miundombinu ya uhakika itakayokidhi mahitaji yote ya wateja wetu popote walipo hapa nchini”, alisema Bw. Sambu.
OCD wa Kinondoni SSP Ally Wendo (wa tatu kulia) akiwa pamoja na wafanyakazi wa SGA Security wakati wanaonesha tuzo ambayo kampuni hiyo ilishinda katika maonyesho ya madini Mkoani Geita hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko Faustina Shoo, Meneja Utawala Holythur Mlambiti na Mkurugenzi Mtendaji Eric Sambu. 
OCD wa Kinondoni SSP Ally Wendo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SGA Security wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na SGA Security.
OCD wa Kinondoni SSP Ally Wendo akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa na walinzi wa SGA Security wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na SGA Security.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...