Msimamizi
wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Saukwa,
akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya usafirishaji, juu ya sheria ya
Afrika Mashariki ya udhibiti wa uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni
zake za mwaka 2018, yaliyofanyika kwa siku moja katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Hakimu
Mkazi Mfawizi mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Sylvia Lushashi akiteta jambo
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga pamoja na Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Kashinde Mussa, baada ya kuahirishwa kwa
semina ya mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 kwa wadau wa
usafirishaji, jijini Dodoma.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 wakimsikiliza
mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira,
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Kashinde Mussa (hayupo
pichani), wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku moja
katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Kashinde Mussa akifunga semina ya mafunzo
kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti
Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za
mwaka 2018 iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...