Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKURUGENZI
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Samwel Warioba amesema
miradi mbalimbali ya kimaendeleo inatarajiwa kutekelezwa kupitia fedha
zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan.
Warioba ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Amesema miradi mbalimbali ya kimaendeleo itafanikishwa kupitia fedha hizo zilizotolewa na Serikali.
Amesema
mji mdogo wa Mirerani wenye kata mbili za Mirerani na Endiamtu zina
wakazi wengi hivyo inatakiwa kujengwa kituo kipya cha afya kwenye kata
ya Mirerani ambayo haina kituo cha afya.
"Ila
kituo hicho cha afya kipya kinapaswa kujengwa kipya kikiwa na eneo na
kuchimbwa msingi na siyo kupandisha hadhi zahanati," amesema Warioba.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Baraka Kanunga amewataka madiwani
wa kata za Mirerani Salome Mnyawi na Endiamtu Lucas Zacharia kukaa
pamoja juu ya mikakati ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Mirerani.
"Mkurugenzi
ameshasema kituo kipya cha afya cha kata ya Mirerani kinapaswa kujengwa
mara moja hivyo kaeni kwa pamoja mfanikishe hilo ili kazi ianze,"
amesema Kanunga.
Diwani
wa kata ya Mirerani, Salome Nelson Mnyawi amesema kata hiyo haina
zahanati wala kituo cha afya cha serikali ila kuna zahanati mbili za
binafsi ya Minja na Moipo zinazohudumia wananchi.
"Wananchi
wa kata ya Mirerani hawana kituo cha afya, tunaiomba halmashauri
itekeleze sera ya serikali ya kuwa na kituo cha afya kwenye kila kata,"
amesema Salome.
Diwani wa
kata ya Endiamtu, Lucas Chimba Zacharia amesema eneo lipo la kujenga
kituo cha afya kwenye kata ya Mirerani, hivyo maandalizi yaanze ili
kituo hicho kianze kujengwa ili kikamilike.
"Ujenzi
wa kituo hicho cha afya kwenye kata ya Mirerani kitapunguza wingi wa
wagonjwa kwenye kituo cha afya kilichopo kata ya Endiamtu," amesema.
Diwani
wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian amesema serikali inapaswa kuunga
mkono jitihada za mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite Saniniu
Laizer aliyejenga shule.
"Bilionea
Laizer amejenga shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza na kuikabidhi
serikali hivyo halmashauri imuunge mkono kwa kujengwa bweni," amesema
Taiko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...