Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dk. Abdallah Salehe Possi amefungua rasmi Onesho la Utalii la My Tanzania Roadshow 2021 lililoanza leo katika mji wa Frankfurt nchini Ujerumani. Onesho hili litafanyika katika nchi tatu zikiwemo Ujerumani, Austria na Switzerland kwa muda wa siku 6 kuanzia 25-30/10/2021 ambapo Ujumbe wa Tanzania wenye jumla ya Kampuni za Utalii 28 pamoja na taasisi za TANAPA na Ngorongoro utakutana Wafanyabiashara ya Utalii (Travel Agents) wapatao 150. Mhe. Balozi Possi ameahidi kutoa ushirikiano wa kuendelea kutangaza utalii kupitia njia mbali mbali ikiwemo mikutano ya kimtandao pamoja na vyombo vya habari ili kuhakikisha idadi kubwa ya watalii kutoka nchi zinazozungumza lunga ya kijerumani wanatembelea Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...