Na Oscar Shikunzi,Michuzi TV
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF )umeidhinisha Sh. billion 5.5 kwa ajiili ya kuondoa athari za kiuchumi zilizochochewa na mlipuko wa UVIKO-19 kwa kaya walengwa 40,740 kwa kuwaondolea umasikini wa kipato kwa kuwapatia ruzuku za kujikimu,ajira za muda na kuwaongezea ujuzi,maarifa na elimu ya ujasiriamali.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleza utekelezaji wa mpango maendeleo kwa ustawi wa Taiga na mapambano dhidi ya uviko-19 leo Oktoba 18,2021 jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga amesema kupitia fedha hizo kaya walengwa 40,740 wenye uwezo wa kufanya kazi ambao wanaishi katika maeneo ya mijini,watafanyakazi katika miradi ya jamii na kulipwa ujira wa wastani wa shilingi 135,000 kwa mwezi.
"Usimamizi utafanyika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango kulingana na thamani ya fedha,ni matumaini yeti kwamba fedha hii iliyotengwa kwaajil ya TASAF itasisimua uchumi wa kaya uliokuwa umedorora kutokana na athari za UVIKO-19 na hivyo kuchangia katika mapambano ya kuondoa umasikini ambayo no sehemu ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa,"amesema Mwamanga.
Aidha amesema kaya maskini wamerudi nyuma kiuchumi na wamepoteza rasilimali zao kama mifugo kwa kuziuza ili kupata fedha ya kujikimu .kufuatia hali hii serikali iliweka mikakati mbalimbali ya kunusuru kaya hizi. moja ya mikakati iliyowekwa ni kutafuta fedha na kutoa rudhuku ya ziada kwa kaya hizi ili kukubaliana na athari zilizotokana na UVIKO-19.
Ladislaus amemaliza kwa kutoa shukran za dhati kwa Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kufanikisha upatikanaji wa upatikanaji wa Fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...