Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Bagamoyo
KAMPUNI ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania(TGDC) ambayo ni kampuni tanzu ya ugavi wa umeme (TANESCO) inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 imefafanua kwa kina shughuli inazofanya katika kuhakikisha inatoa mchango wake katka kuzalisha umeme unaotokana na jotoardhi.
TGDC imetoa ufafanuzi wa shughuli zake kupita mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini kwa waandishi wa habari nchini ambao wamepiga kambi wilayani Bagamoyo wakiendelea kunoelewa kuhusu nishati jadidifu huku warsha ikiongozwa na mada inayosema Nishati Jadidifu kwa Maendeleo ya Uchumi na Jamii.
Akizungumza wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari Mhandisi Cynthia Kuringe kutoka TGDC amesema kampuni hiyo ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongoza maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania.Kampuni ilianza shughuli zake Julai 2014.
Akieleza kwa kina kuhusu TGDC, Mhandisi Kuringe amesema kampuni hiyo inalojukumu na mamlaka ya kutafiti ,kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi nchini katika kuzalisha umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.
Kuhusu lengo la kuanzishwa kwa TGDC,Mhandisi Koringe amesema kwa miongo mingi Tanzania imekabiliwa na tatizo la upungufu wa wa uzalishaji wa umeme wa kutosha kutokana na sababu mbalimbali.Serikali iliamua kuwa na vyanzo vya uzalishaji wa umeme vya nishati jadidifu vikiwemo jua, upepo na jotoardhi."Hatua hizo ndizo zilizosababisha kuanzishwa kwa TGDC."
Mhandisi huyo amesema dira yao ni kuwa kampuni ya maendeleo ya jotoardhi inayoongoza na yenye ushindani katika ukanda huu, kuhudumia kizazi cha na baadae kwa nishati ya uhakika,yenye gharama nafuu na rafiki wa mazingira.
Wakati dhamira ya TGDC ni kutoa huduma za maendeleo ya nishati ya jotoardhi za uhakika na ufanisi,kusaidia dira ya maendeleo ya Taifa, kuongeza ajira mpya kwa watanzania pamoja na kuongeza uelewa na njia mbalimbali za matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.
Kuhusu hali ya jotoardhi nchini Tanzania ikoje,amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopo katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki na kujaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za nishati za jotoardhi kukadiriwa kuwa na zaidi ya megawati 5000.
Aidha amesema hadi sasa kuna maeneo zaidi ya 52 yenye viashiria vya nishati jotoardhi Tanzania ,kutokana na tafiti za awali za kisayansi hali hiyo inaashiria kuna hifadhi kubwa ya nishati ya jotoardhi.
"Hadi kufikia 2018 Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania(TGDC) ilikuwa imefanya tafiti katika maeneo ya Songwe, Ngozi-Mbeya,Mbaka Kiejo-Mbeya, Luhoi-Pwani, Ibadakuli-Shinyanga, Kisaki-Morogoro, Natroni-Arusha na Meru mkoani Arusha,"amesema.
Pia amesema kuna hatua ambazo hupitiwa kabla ua uvunaji ama kabla ya kuanza kunufaika na matumizi ya nishati jotoardhi.Hatua hizo ni utafiti juu ardhi, tafiti za kina,uchorongaji wa visima ya kusafirisha nishati, ujengaji wa mitambo ya kuzalisha umeme, kuanza uzalishaji na ufunguzi.
Alipoulizwa ni kwa kiasi gani nishati ya jotoardhi huzalisha umeme, amejibu mvuke ukiwa kwenye juzi joto 107 hadi 300 hutumika kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia mbalimbali ,mitambo ya kuzalisha umeme huzungushwa na mvuke unatoka ardhini katika mkandamizo mkubwa.
Pamoja na hayo Mhandisi Koringe amesema TGDC imeweka malengo yake ya kuhakikisha hadi ifikapo mwaka 2025 wawe na uwezo wa kuzalisha megawati 200 za umeme unaotokana na nishati ya jotoardhi ili kuchangia malengo ya Serikali iiyodhamiria kuwa na umeme unaotokana na nishati jadidifu.
Profesa Majombo kutoka Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...