Mkurugenzi wa program unganishi ya walinzi binafsi nchini (Tpsis) David Rwegoshola akizungumza na viongozi wa Kata ya Wazo na Kilimahewa juu wakati wa kukabidhiwa rasmi Kata hizo kwa ajili ya kupambana na vijana walioshindikana ( vishandu)
Miongoni mwa Askari kutoka program unganishi ya walinzi binafsi nchini (Tpsis) wakiwa tayari kuingia mitaani kutoa Elimu shirikishi na ulinzi shirikishi.
Mwenyekiti wa wenyeviti katika Kata ya Wazo Mashauri akizungumza na Michuzi kwa jinsi gani raia wakigeni wamekua wakiingia katika Kata hiyo kama chimbo lao la kufanya uhalifu na kupora mali za raia.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama katika Kata ya Wazo,Husna Nondo akiwa na Mkurugenzi wa program unganishi ya walinzi binafsi nchini (Tpsis) David Rwegoshola wakipasha miili joto kwenye gwaride la Askari ambao watapambana na wahalifu katika Kata ya Wazo na Kilimahewa juu.

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KATA ya Mtaa wa Kilimahewa juu ikishirikiana na Kata ya Wazo kupitia programu unganishi ya walinzi binafsi nchini wahaidi kwa kuboresha na kulinda usalama wa raia na Mali zao.

Akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa kupokea Makamanda ambao wataungana na viongozi wa Kata ya Wazo pamoja na Kata ya Kilimahewa juu ,Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ambae pia ni Mtendaji Mkuu wa Kata ya Wazo Husna Nondo amesema kuna Maeneo ambayo yamekua yakifanywa ni sehemu ya machimbo ya uhalifu inayopelekea kuzalishwa kwa vibaka,waporaji na wezi wa mifugo .

"Ni Kata kubwa mno hivyo utaona hata mkusanyiko wa watu ni mkubwa Lakini kutokana na kuwepo uhalifu inapelekea hata watu kushindwa kufanya Maendeleo kwa kuhofia usalama wao na Mali zao hasa Maeneo ya Kilimahewa juu na kata ya Wazo yenyewe."

Hata hivyo Nondo amewapongeza programu unganishi ya walinzi binafsi nchini (Tpsis) kwa kuona ipo haja ya kutoa ulinzi shirikishi na elimishi kwa kata ya Wazo ili kusaidia kuboresha usalama wa raia na Mali zao.

"Kupitia muunganiko huu tunategemea kukomesha na kutokomeza uhalifu katika Kata zetu ili kuweza kufanya Maendeleo na kuona Kata zetu ni sehemu ya uwekezaji."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa program unganishi ya Walinzi binafsi nchini (Tpsis) David Rwegoshola amesema ni vyema jamii ikatoa Elimu shirikishi kwa vijana ambao tayari wameshajiingiza kwenye vitendo viovu ili kuangalia kwa jinsi gani wataweza kubadili taswira za vijana hao kuwa Maisha ya uhalifu ni ya utajiri .

"Vijana wengi hasa wahalifu wanaamini kuwa ukijiingiza kwenye vitendo viovu ndio umetoboa Maisha au kufanikiwa lakini Hali hii ikiweza kudhibitiwa na jamii kuonyesha jitihada za kutoa Elimu shirikishi tunaweza kutokomeza kabisa vitendo vya uhalifu wa kila aina."

Pia ameeleza kwa namna gani Askari hao 90 ambao wamehaidi kuboresha usalama katika Kata ya Kilimahewa juu na kata ya Wazo na kupitia programu unganishi wataweza kupambana na vijana walioshindikana .

"Ni Askari ambao wataboresha ulinzi na usalama katika Kata hii na tunategemea kazi itafanyika ya kusafisha na kupewa Ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi wenyewe na kutoa taarifa sehemu zenye magenge ya vibaka,Wala unga,Majambazi na Wale wanaojiita vishandu."

Nae Mwenyekiti wa wenyeviti katika Kata ya Wazo Medard Mashauri ameongeza kuwa Kutokana na ukubwa wa Kata ya Wazo hata watu nao wamekuwa wengi na kupelekea wageni kuingia katika Makazi na kufanya uhalifu.

"Raia wakigeni hasa kabila la wanyasa kutoka nchi ya Malawi wamekua wakijihusisha na uhalifu wa kuvunja maduka kwa kutumia tindikali,Kata ya Wazo Ina wakazi wengi na Miongoni mwao wanapata posho kupitia raia hao wakigeni na Kutunza Siri sawa na kuwapatia uhakika wa Kuishi sehemu hiyo."

Hata hivyo ameongeza kuwa ujio wa Makamanda hao utakua chachu ya kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wanatoa Elimu kwa kuwapa vijana muongozo jinsi ya kutafuta kipato Cha halali pasipo kujiingizia kwenye vitendo vya uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...