MAANDALIZI kwa ajili ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager marathon kwa mwaka wa 2022 yanaendelea vizuri huku usajili ukishika kasi mara tu baada ya kufunguliwa.

Hayo yamethibitishwa na waandaaji wa mbio hizo, ambapo wamebainisha kuwa punguzo la bei la asilimia 20 katika kujisajili bado unaendelea.

 Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam, usajili bado unaendelea kufanyika kwa njia ya mtandao wa Tigopesa kwa kupiga *149*20#, sambamba na tovuti rasmi ya Kilimanjaro Marathon-www.kilimanjaromarathon.com.

Taarifa hiyo pia iliwakumbusha wanaotarajia kushiriki kutumia fursa ya muda wa punguzo gharama za kujisajili ambao umeanzia Oktoba 17, mwaka huu na unatarajia kufikia kikomo Januari 7, mwakani.

"Baada ya muda wa punguzo kumalika hakutakuwa na punguzo tena, badala yake washiriki watalazimika kulipa ada ya kawaida ya usajili,” ilieleza na kusisitiza kuwa masuala yoyote kuhusu bei yanatangazwa kwenye kurasa maalumu tu za mtandao za Kilimanjaro marathon na vyombo vya habari na sio kwingineko.

Waandaaji hao wameendelea kutoa ushauri kwa wanaotarajia kushiriki mbizo kujiandikisha mapema ili waandaaji wapate nafasi ya kujitayarisha mapema zaidi.

"Usajili wa mapema pia utatupa sisi wandaaji nafasi ya kufanya matayarisho yanayohusiana na washiriki kama vile huduma za maji, magari ya wagonjwa, matunda na medali kwa vile tutakuwa na idadi yao mapema,” ilielezea sehemu ya taarifa hiyo.

 Taarifa hiyo pia imewakumbusha washiriki kuwa Kilimanjaro Premium Lager Marathon itaadhimisha Miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, hivyo itakuwa ni tukio maalum, kubwa na la kipekee, hivyo ni vyema mtu akashiriki tukio hilo la kihistoria.

Wadhamini wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni pamoja na Kilimanjaro Premium Lager - 42km, Tigo Kili Half Marathon - 21km na Grand Malt kilomita 5, ambapo wadhamini wa meza za maji kwa ajili ya washiriki ni Absa Tanzania, Unilever, Simba Cement, Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd, Kilimanjaro Water na TPC Sugar sambamba na watoa huduma maalumu ambao ni pamoja na GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel na CMC Automobiles.

Mbio za Kilimanjaro Marathon, zinazotarajiwa kufanyika katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU) Februari 27, 2022m huandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon na kuratibiwa kitaifa na Kampuni ya Executive Solutions.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...