Hafsa Omar-Dodoma

Wataalam kutoka Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wa kutoka katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamefanya kikao cha Ushirikiano kwa ngazi ya wataalam.

Kikao hicho cha Ushirikiano baina ya Wizara hizo kimefanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Kikao hicho, kimeongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC), Mikidadi Rashidi na kuhudhiriwa na Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake pamoja na wajumbe kutoka katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Taasisi zilizopo chini yake.

Wajumbe wa kikao, walijadili ajenda mbalimbali ambazo ni hatua zilizofikiwa katika kukamilisha hati ya Mashirikiano(MoU) kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Mamlaka ya Udhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Asilia, Zanzibar (ZPRA), hatua iliyofikiwa katika kukamilisha hati ya mashirikiano (MoU) kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC) na masuala mengine mbalimbali.

Wakati akifungua kikao, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu, aliwataka wajumbe hao kutoa michango yao kwa ufanisi.

Kikao hicho ni moja ya vikao ambavyo vinafanyika kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na Ofisi ya Makamu  wa Rais, ambavyo hupaswa kufanyika mara nne kwa mwaka.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu ( mbele-kushoto), Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC), Mikidadi Rashidi(mbele-kulia) wakiendesha kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara hizo kilichofanyika Oktoba 27,mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma
Washiriki Kutoka Wizara  ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Taasisi zilizopo chini yake wakiwa katika  kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.


Picha mbalimbali za matukio katika kikao na baada ya kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...