Na Humphrey Shao, Michuzi TV.
FAMILIA ambazo zimekuwa zikiishi na wafanyakazi wa ndani au ambao wanakata kuwa na wafanyakazi hao wameshauriwa kutoa mikabata ambayo itasaidia haki kutendeka kwa pande zote mbili inapofika hatua
Akizungumza na Michuzi TV , mmoja ya wafanyakazi wa ndani ambaye amefanikiwa kupata mkataba Ramla Nassoro(18) amesema mfanyakazi akiwa na mkataba inafanya kuwa uhakika na maslahi yake hata anapoamua kuacha au kuachishwa kazi.
Baadhi ya wasichana wa kazi za nyumbani katika Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam wameanza kupatiwa mikataba ya kazi na waajiri wao ili kulinda usalama wa ajira zao.
Ramla amesema baada ya kuhudhuria semina ambayo alishiriki na mwajiri wake, ndiyo iliyosababisha apewe mkataba."Mkataba nimeridhika nao na nimefarijika kwa sababu sasa hivi naishi na kufanya kazi kwa uhuru.
"Najua haki zangu na majukumu yangu, nawashauri waajiri wengine kuwapa mikataba ya kazi wafanyakazi wao," amesema Ramla.
Kwa upande wake Mwajiri wa msichana huyo, Asha Dilangala amesema alihamasika kumpa mkataba mfanyakazi wake baada ya kuelimishwa kuhusu umuhimu wa mkataba wa kazi kwani unamlinda mfanyakazi na mwajiri.
"Nilimruhusu msichana wangu kwenda kupata mafunzo alivyorudi alinieleza aliyojifunza akaniambia kwamba tunatakiwa tuishi kimkataba. Mimi niliona ni jambo sahihi nilimchukulia kama mfanyakazi mwingine nikaamua kumuandalia mkataba," amesema.
Hatua hiyo ni matokeo ya mradi wa Wezesha Uelewa wa Haki zuia rusha ya ngono ndani ya jamii unaotekelezwa na Sauti ya Jamii Kipunguni na kufadhiliwa na Women Fund Tanzania Trust.
Kupitia mradi huo Sauti ya jamii ya Kipunguni iliendesha mafunzo kwa wafanyakazi wa kazi za majumbani juu ya uelewa wa haki, madhara ya rushwa ya ngono na kuripoti vitendo vya ukatili kwenye mamlaka husika.
Amesema anaendelea kuwahamasisha waajiri wengie wenye wasichana wa kazi za ndani waweze kuwapatia mikataba ili waishi kwa amani na uhuru.
Ratifa Mussa ambaye pia alihudhuria mafunzo hayo amehamasika kwa kuanza kuwapa elimu wasichana wengine watambue haki zao na kutambua madhara ya rushwa ya ngono.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii Kipunguni Selemani Bishangazi, amesema walitoa semina ya madhara ya rushwa ya ngono na uelewa wa haki kwa wadada wa kazi 120 kutoka Kata ya Kipunguni.
"Wafanyakazi wa majumbani wana haki ya kuthaminiwa ndiyo maana tunawahamasisha wawe na nguvu ya kupambana na unyanyasaji kwa sababu wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu na hawana mikataba ya ajira," amesema Bishangazi.
Mradi huo unalenga kuendeleza kampeni ya kuzuia rushwa ya ngono kwa wafanyakazi wa kazi za majumbani na wanawake wenye ndoto za kuwa viongozi, umuhimu wa kuripoti vitendo vya ukatili kwenye mamlaka husika na kudai haki na kuwajibika.
Mmoja wa wafaidika wa Mafunzo ya wadada wankazi akitoa Mafunzo kwa wasichana wengine wa Kata ya chanika
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...