Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililozinduliwa usiku wa kuamkia  jana Oktoba 28, 2021, litaendelea na sasa ahadi imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa katika viwanja vya TaSuBa mjini Bagamoyo  kuwa Wizara hiyo sasa ni ya moto na haitapoa,Kazi iendelee.

Katika Tamasha hilo lililohudhuriwa na maelfu ya watu kutoka mikoa na maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi na kupata burudani kutoka wasaniii mbalimbali, Waziri Bashungwa alisema ubunifu na nia ya kutaka sekta hizo za ubunifu kulisafia Taifa katika ajenda za maendeleo za Rais wetu Samia Suluhu Hassan ndio nguzo kuu kwa sasa.

Wasanii kadhaa walitumbuiza na kuwakonga nyoyo vilivyo viongozi waliokuwepo sambamba na baadhi ya mabalozi  waliokuwepo kutoka nchi za Japan, India, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Naibu Waziri wa Utamaduni, Pauline Gekul, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah ambao mara kadhaa hawakusita kunyanyuka na kwenda kucheza.

Tamasha hilo linaendelea leo Oktoba 29, 2021 kwa maonesho na kisha jioni burudani mbalimbali, ambapo leo kwa upande wa muziki wa kizazi kipya wasanii kadhaa wa hip hop na rap watapata fursa katika usiku unaoitwa “AFRICAN MESSAGING NIGHT”

Tamasha hilo linatarajiwa kufungwa kesho usiku Oktoba 30, 2021, kwa “Singeli Night” na linatarajiwa kushuhudiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete.

Aidha, kesho asubuhi tarehe 30 Oktoba wasanii na viongozi mbalimbali watafanya kile kinachoitwa “Bagamoyo Royal Tour” kwa kutembelea vivutio vya utalii. 

Wasanii waliotumbuiza jana ni Beka Flavour, Isha Mashauzi, Saada Nassor kutoka Zanzibar, Saraphina na Ruby.




Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Zainab Abdallah akimvalisha kofia msanii wa bongofleva aitwaye kwa jina kisanii Bela Flevor katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSuBA) mjini Bagamoyo.PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-MMG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Zainab Abdallah wakionesha manjonjo ya kucheza jukwaani  katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSuBA) mjini Bagamoyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akionesha manjonjo kwa kucheza muziki katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA) mjini Bagamoyo.
Mrisho Mpoto akinogesha usiku wa tamasha hilo 
Shangwe mikono kama yotee.
Msanii wa Taarabu Isha Mashauzi akitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSuBA) mjini Bagamoyo.
Msanii wa Taarabu Isha Mashauzi akituzwa na shabiki jukwaani katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo mjini Bagamoyo.









Msanii Ruby akiimba jukwaani kwa hisia
Shangwe tuu



Msanii wa muziki wa Kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Beka Flevor  akitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Tamaduni Bagamoyo lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Oktoba 28, 2021 katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSuBa) mjini Bagamoyo.
Shabiki akijimwaya mwaya kwa raha zake
Mashabiki wa muziki wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri usiku huo
Shabiki akionesha umahiri wake wa kucheza jukwaani muziki wa kimwambao












 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...