Akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha, Prof.Mbarawa ameitaka bodi hiyo kuendelea kutumia fursa waliyonayo kwa kuwajengea uwezo wataalamu wanafunzi.
Aidha amezitaka taasisi zenye mamlaka kuhakikisha wataalam wanaopewa dhamana ya kutekeleza miradi wanazingatia sheria katika upatikanaji na uendeshaji wa ujenzi ambapo amewataka wataalamu hao kuwa waadilifu na wazalendo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Kwa upande wake rais wa Chama cha Ubunifu Tanzania na Chama cha Ubunifu majengo Afrika Mashariki David Kibebe katika mkutano huo amesema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni ushirikishwaji Mdogo wa Sekta binafsi katika miradi ya serikali.
Naye Msajili wa Bodi ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi Arch.Edwin Nnunduma amesema hadi kufikia septemba mwaka huu jumla ya wataalam 1188 na makapuni 411 yamesajiliwa na kuwafuta wataalam 132 na Makampuni 72 kutokana na makosa tofauti tofauti.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Pro.Makame Mbarawa akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta ya unjenzi, uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Msajili wa Bodi ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi Arch.Edwin Nnunduma akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe: Pro.Makame Mbarawa.
Rais wa Chama cha Ubunifu Tanzania na Chama cha Ubunifu majengo Afrika Mashariki David Kibebe akitoa hotuba yake wakati wa mkutano huo.
Msajili wa Bodi hiyo, Arch.Edwin Nnunduma, (kulia aliyesimama) akifafanua jambo.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wakifuatilia mada mbali mbali.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Pro.Makame Mbarawa akiangana na watumishi wa Bodi ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) alipotembelea banda hilo kujionea shughuli zinazofanywa na bodi hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Pro.Makame Mbarawa akisalimiana QS. Bundala Mashaka alipowasili kufungua mkutano wa wataalamu wa sekta ya unjenzi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano AICC Arusha. (wa kwanza kushoto) Msajili wa Bodi hiyo Arch.Edwin Nnunduma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Pro.Makame Mbarawa akisalimiana na Rais wa Chama cha Ubunifu Tanzania na Chama cha Ubunifu majengo Afrika Mashariki David Kibebe alipowasili kufungua mkutano wa wataalamu wa sekta ya unjenzi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano AICC Arusha.
Washiriki wa mkutano wakiwa nje ya ukumbi wakihakiki majina yao kabla ya kuingia katika mkutano.
Habari Picha na / Philemon Solomon
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...