NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MABINGWA  wa Jamhuri mwaka 1988 African Sports “Wanakimanumanu” wameanza kuzipigia hesabu pointi tatu kwenye mchezo wao wa Champion Ship dhidi yao na JKT Tanzania utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya timu ya African Sports  Said Karsandas (Pichani ) alisema kwamba maandalizi kwa upande wao yamekamilika kwa asilimia 90 huku wachezaji wakiwa na hari kubwa kuelekea mchezo huo.

Alisema kwamba pamoja na maandalizi ambayo wameyafanya lakini wataingia kwenye mchezo huo kupambana kufa na kupona kutokana na aina ya timu ambayo wanakutana nayo yenye uzoefu katika soka .

“Tunatambua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu kutokana na kwamba wapinzani wetu aina ya rasilimali zote na wana wachezaji asilimia 90 walioshuka nao daraja lakini tunaamini kwamba tutaingia kwa lengo la kwenda kupambana ili tupate matokeo”Alisema

Alisema kwamba licha ya kwamba matokeo sio mazuri kwa upande wao kutokana na wameshinda mchezo mmoja, sare mitatu wakiwa na pointi sita huku wakiwa wamepoteza michezo mwili lakini watapambana hadi kieleweke.

“Mechi hii ni ya kufa na kupona ushindi kwetu ni muhimu kutokana na kwamba utaturudisha kwenye nia sahihi na malengo tuliojiwekea kwenye msimu huu kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kila mechi”Alisema

Hata hivyo aliwataka wapenzi, mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ambao utakuwa wa aina yake huku akieleza hizo ni mbio za kupokezana vijiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...