BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya
Jubilee Insurance wamezindua huduma ya bima maalum ya kilimo inayolenga
kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi
wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao.
Bima
hiyo ilizinduliwa mapema hii leo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga na
Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Erasto Kiswaga katika hafla fupi ambayo pia
ilihusisha mafunzo kuhusu umuhimu na faida za Bima hiyo kwa wadau
mbalimbali wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS)
kutoka mkoa huo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi wa
Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke
alisema ujio wa huduma hiyo ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo
katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini kupitias huduma za kibenki
zinazolenga kutatua changamoto zinazogusa sekta hiyo muhimu.
“Benki
ya NBC tuinatambua vema sekta ya kilimo na zaidi tunatambua mchango wa
wa wakulima katika uchangiaji wa uchumi wa nchi na kwa msingi huu
tumeona ni vema kuja na Bima ya mazao kwa wakulima. Bima hii ni ya
kwanza nchini na tunaamini kwa dhati kwamba kupitia bima hii wakulima
watapunguza kwa kiwango kikubwa hasara zitokanazo na majanga mbalimbali
yasiyotabilika yaani yale yalio nje ya uwezo wao.’’ alisema
Alisema
ujio wa huduma hiyo utawasaidia watanzania ambao asilimia 70
wanategemea shughuli ya kilimo kwa kuwapatia uhakika wa matokeo
wanayoyatarajia kupitia shughuli zao za kilimo, uvuvi na ufugaji hata
pale wanapokabiliwa na majanga ya asili ikiwemo mvua ya mawe, mafuriko,
ukame, upepo mkali, moto na majanga mengine ambayo yamekuwa
yakiwasababishia hasara kubwa na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw Erasto Kiswaga alitoa
wito kwa wakulima hao kutumia fursa hiyo kukata bima ili iwasaidie
kuwakinga wanapokumbwa na majanga mbalimbali huku akiitaja sekta ya
kilimo kuwa miongoni mwa sekta zinazokabiliwa na majanga mengi
yasiyotabirika ikiwemo mafuriko, moto, wadudu na ukame ambavyo vimekuwa
vikiwasababishia hasara kubwa wakulima.
“Hizi ni dalili njema
kuona sasa huduma za Bima zimeanza kuwafikia wakulima ambao kimsingi
ndio kundi kubwa zaidi katika shughuli za uzalishaji hapa nchini
likigusa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania. Nitumie fursa hii kuwaomba
viongozi wa vyama vya msingi mliohuduhuria uziunduzi huu vipelekea
mpango huo kwenye bodi za mazao mbalimbali ili utaratibu wa kuwalipia
bima hii wakulima uanze mara moja,’’
“Kama ambavyo wananchi
wamekuwa wakitaka bima nyingine ikiwemo bima za magari ni vema pia wawe
na bima kwa ajili ya mazao yao kwa kuwa kuanzia hii leo hasara kwenye
kilimo imepata tiba,’’ alisema.
Hii ndio sababu nawapongeza
benki ya NBC kwa kulifikia kundi hili. Kikubwa sasa nawaomba sana NBC
kwa kuzingatia umuhimu wa mpango muweze kuwafikia wakulima wote ili
wanufaike na huduma hii muhimu,’’ alisema.
Awali akifafanua
zaidi kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki hiyo Bw
Benjamini Nkaka alizitaja bima hizo kuwa ni pamoja na bima ya Mazao
inayohusisha mazao yote ya chakula na biashara pamoja na mazao ya
matunda, Bima ya Mifugo inayohusisha mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi
kondoo pamoja na Bima ya samaki mahususi kwa ajili ya wavuvi.
“Pamoja
na Bima hizo pia tuna Bima ya Misitu inayolenga kumkinga mkulima wa
miti dhidi ta majanga kama moto, milipuko na majanga mengine ya asili
yanapotokea na kuleta hasara ambapo kupitia huduma hii mkulima ataweza
kupata fidia,’’ alifafanua Bw Nkaka huku akibainisha kwamba bima zote
hizo zitazotolewa kwa ada ya asilimia 7 ya thamani ya zao husika.
Zaidi,
akitaja baadhi ya faida zitokanazo na bima hiyo ambayo tayari
imeshaanza kutolewa kwa wakulima wa mazao ya tumbaku kwenye mikoa ya
Tabora, Kigoma na wilaya ya Kahama, Bw Nkaka alisema inatoa fidia kwa
wakulima na wafugaji pindi wapatapo hasara zitokanazo na majanga
mbalimbali na inawapa wakulima na wafugaji uhuru na amani ya kuendelea
na shughuli za kilimo bila kuhofia hasara
“Zaidi bima hii
inamnufaisha mkulima na mfugaji katika kulinda kipato chake, bila kurudi
nyuma hasara inapotokea na hivyo kuwa na kilimo endelevu na pia
itamuwezesha mkulima na mfugaji kujifunza zaidi hatua bora za ufugaji na
ukulima.’’ Alisema akiongeza kuwa mkulima anaweza kupata bima hiyo kwa
kiwango cha chini hadi kufikia Tsh 25,000 kwa hekari moja kwa mazao
yote.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao Mwenyekiti wa Chama
Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU) na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Bw
Emmanuel Cherehani alisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka katika
kipindi ambacho wakulima wamejipanga kufanya mapinduzi ya kilimo kupitia
kilimo cha kisasa kinachoshusisha tahadhari zote muhimu ili kuepuka
hasara ambazo zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimaendeleo.
“Ni
msimu uliopita tu wakulima tulipata hasara ya dola laki mbili katika
wilaya ya Kahama tu kutokana na majanga haya. Ni kutokana na hasara kama
hizo ninaomba vyama vya msingi viangalie namna ya kuwalipia wakulima
bima hizi kupitia mjengeko wa bei ili wote wawe na bima badala ya
kusubiri benki ndio ianze kukimbizana nao huko,’’ aliagiza.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Bw Erasto Kiswaga (katikati) akiongoza zoezi la
uzinduzi wa huduma ya bima maalum ya kilimo ya Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC) inayolenga kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini
dhidi ya hasara pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri
uzalishaji wao wakati wa hafla iliyofanyika Wilayani Kahama, Shinyanga
mapema hii leo. Wengine ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja
binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa pili kushoto), Naibu Mrajisi
wa Vyama vya Ushirika Bw Augustine Semkurutu (wa pili kulia),
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Bw
Kwiyolecha Mkilijiwa (kushoto) na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika
wa Tumbaku (WETCU) Bw Hamza Kitunga (Kulia)
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Bw Erasto Kiswaga akizungumza na wadau mbalimbali
wa kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS)
kutoka mikoa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma ya bima maalum ya
kilimo ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) inayolenga kuwalinda
wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi wanapopata
majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao wakati wa hafla
iliyofanyika Wilayani Kahama, Shinyanga mapema hii leo.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki
Masuke akizungumza na wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima na
viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) kutoka mikoa mbalimbali wakati wa
uzinduzi wa huduma ya bima maalum ya kilimo ya Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC) inayolenga kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini
dhidi ya hasara pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri
uzalishaji wao wakati wa hafla iliyofanyika Wilayani Kahama, Shinyanga
mapema hii leo.
Akizungumza
kwa niaba ya wakulima hao Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama
(KACU) na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Bw Emmanuel Cherehani (pichani)
alisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka katika kipindi ambacho
wakulima wamejipanga kufanya mapinduzi ya kilimo kupitia kilimo cha
kisasa kinachoshusisha tahadhari zote muhimu ili kuepuka hasara ambazo
zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimaendeleo.
Mkuu
wa Idara ya Bima wa Benki hiyo Bw Benjamini Nkaka akizungumza na wadau
mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi
(AMCOS) kutoka mikoa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma ya bima
maalum ya kilimo ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) inayolenga
kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi
wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao wakati
wa hafla iliyofanyika Wilayani Kahama, Shinyanga mapema hii leo.
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Bw Kwiyolecha
Mkilijiwa akitoa neon la shukrani kwa benki ya NBC kwa ajili ya huduma
hiyo kwa wakulima.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) Bw Hamza Kitunga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wadau
mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi
(AMCOS) kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya bima
maalum ya kilimo ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) inayolenga
kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi
wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao wakati
wa hafla iliyofanyika Wilayani Kahama, Shinyanga mapema hii leo.
Home
HABARI
Benki Ya NBC Yazindua Bima ya Kilimo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, Serikali yaunga mkono
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...