MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wajibu, Ludovick Utouh, amesema bila ya kuwepo kwa uwazi katika utendaji wa serikali, uwajibikaji hautakuwepo, ili uwajibikaji uwepo, ni lazima kwanza utanguliwe na uwazi, baada ya kuwepo kwa uwazi kwa kila mtu kujua kila kinachofanyika, watendaji watajikuta wanalazimika kuwajibika maana kila kitu kitakuwa kiko wazi.
Utouh ameyasema hayo, jijini Dodoma, katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, wakati akilitambulisha kongamano la kimataifa la ITAC, kujadili umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika kusukuma mbele maendeleo, sio tuu ya nchi ya Tanzania, bali maendeleo ya bara lote zima la Afrika.
Bwana Utouh, amesema Kongamano hilo la siku mbili, linafanyikia jijini Arusha, litaanza kesho Alhamisi, tarehe 18 November, 2021 na kumalizika Ijumaa, tarehe 19, November, 2021 ambapo mada mbalimbali kuhusu umuhimu wa uwazi na uwajibikaji, zitawasilishwa na wataalamu wabobevu wa kimataifa kutoka Tanzania, Afrika na Kimataifa.
Bwana Utouh amesema, kongamano hilo lina umuhimu wa kipekee, kwasababu bila kuwa na uwazi katika utendaji kazi serikalini, utendaji unakuwa haupo, na kusisitiza, hoja za uhitaji wa serikali kutenda kazi kwa uwazi, ni takwa la kikatiba, na lipo kwenye katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Jumla ya washiriki 500 kutoka sehemu mbalimbali, wanatarajiwa kushiriki kongamano hilo, ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamo wa Rais.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...