Na Amiri Kilagalila,Njombe
Bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini (REA) imeshindwa kuridhika na hatua za usambazaji wa umeme kwa wananchi wa kata ya Luponde halmashauri ya mji wa Njombe kutokana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa zoezi hilo na kupelekea kufikia wateja wachache.
Mwenyekiti wa bodi hiyo wakili Julius Bundala Kalolo amesema licha ya hatua nzuri iliyofikiwa na mradi wa Luponde Hydro Power and Rural Electrification Project katika kuendeleza mradi huo na kupata dhamana ya kuwasambazia wananchi nishati lakini zoezi la uunganishaji wa umeme kwa wateja upo nyuma ukilinganisha na matarajio.
“Changamoto kubwa ambayo tumeiona ni kwamba uunganishaji wa wateja uko nyuma,tulitarajia mpaka sasa wateja 1400 tayari wangekuwa wameunganishwa kupitia mradi huu lakini mpa sasa hivi ni 402 tu kwa hiyo karibu wateja 1000 hawajaunganishwa na leo ni mwaka wanne tangu mradi uanze”alisema Bundala
Bundala ameongeza kuwa “tunajua kuweka miundombinu kama hii ni gharama kubwa na inachukuwa muda kufikisha maeneo mbali mbali lakini tulitarajia basi walau hatua iwe imepigwa kwamba zaidi ya nusu wawe wameunganishwa umeme”alisema wakili Julius Kalolo
Vile vile amesema kwa kuwa wamebaini changamoto kubwa inatokana na uchumi wa wakazi wa maeneo hayo,bodi imeelekeza mambo mawili kufanyika ikiwemo kuwafikishia umeme wa UMETA wananchi unaouzwa kwa shilingi elfu thelathini na sita.
“Tumeelekeza mambo mawili yafanyike la kwanza kwa kuwa tumeona nyumba nyingi hazizidi vyumba vinne hii habari ya kuleta wakandarasi kusuka nyaya haina maana na kupitia miradi yetu ya wakala vijijini tuna vyombo vinaitwa UMETA ambazo TANESCO pia wanazo zinauzwa shilingi elfu 36 kwa hivyo nimekubaliana na mkurugenzi mkuu wa wakala wa nishati vijijini ziletwe ili watu wasifikilie mpaka kutafuta mtu wa kusuka waya ndani ya Nyumba”alisema wakili Julius Kalolo
Maxwell Mugombe ni mhandisi wa mradi wa Luponde Hydro Power wenye miradi miwili itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha takribani Jigawatts 17 kwa mwaka,amesema kupitia ufadhiri ambao wamekuwa wakiupata ikiwemo kutoka REA wamefanikiwa kusambaza umeme vijiji saba hivyo licha ya wateja wachache kuunganishiwa mpaka sasa lakini wanajivunia mafanikio ambayo wanaendelea kuyapata wateja wao.
“Sasa hivi tumeunganisha wateja 402 na kati ya hao wapo wa viwanda vidogo,viwanda vya kusaga mahaindi,kulanda pamoja na ofisi za kijiji,shule na zahanati kupata umeme na hilo ndio lengo la mradi wetu”alisema Maxwell Mugombe
Kwa upande wake mhandisi Jones Olotu mkurugenzi wa huduma za ufundi wa wakala wa nishati vijijini (REA) amesema mkoa wa Njombe una jumla ya vijiji 381na vijiji 279 kati ya hivyo vikiwa vimekwishafikiwa na umeme huku vijiji 102 vikiwa havijafikiwa na huduma ya nishati na tayari vimekwisha ingizwa kwenye mpango wa REA 111 mzunguko wa pili.
“Tayari yupo mkandarasi na tumemshampa vijiji vyote 102 kwa atatekeleza kwa miezi 24 na ikifika disember 22 tutakuwa tumemazliza vijiji vyote vya mkoa wa Njombe kwa 100% na tutabakiwa na vitongoji 1750 kwa mkoa mzima na ni vitongoji 822 tu vina umeme mpaka sasa hivi na tayari tumeshaviingiza kwenye mpango”alisema Jones Olotu
Aidha amesema mkoa wa Njombe una maporomoko mengi ya maji na tayari serikali imewawezesha takribani wawekezaji binasi saba wanaozalisha umeme kwa maporomoko ya maji badala ya kutegemea TANESCO tu ili kuwafikishia wananchi huduma ya umeme.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo diwani wa kata ya Luponde bwana Yulick Msemwa ameishukuru serikali kwa kuwawezesha wawekezaji hao kupitia REA kwa ktoa zaidi ya dora laki nane na arobaini na kupelekea kila kijiji kuwa na umeme unaowezesha kuongeza shughuli za maendeleo huku wakiomba kufikishiwa maeneo ambayo bado hayajafikiwa ili wananchi wote waweze kuwa na nishati.
Bodi ya wakurugenzi wakala wa nishati vijiji REA kwa kuambatana na wadau wa maendeleo kutoka umeoja wa Ulaya na ubalozi wa Sweeden pamoja na viongozi kutoka TANESCO wamehitimisha ziara ya siku nne mkoani Njombe kwa kutembelea mradi wa Luponde Hydro kwa lengo la kukagua na kujiridhisha namna miradi ya umeme ilivyoleta manufaa kwa wananchi wa kawaida,kupata mrejehesho wa pesa zilizotolewa na serikali pamoja na wafadhili kama zimetumika kikamilifu kwenye miradi.
Baadhi ya wataalamu kutoka REA,bodi ya wakurugenzi na wataalamu mbali mbali kutoka TANESSO wakipata maelezo kadhaa kutoka kwa mhandisi wa mradi wa Luponde walipotembelea mradi huo.
Wajumbe wa bodi,REA,TANESCO na wageni mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa Luponde Hydro uliopo halmashauri ya mji wa Njombe
Mwenyekiti wa bodi hiyo wakili Julius Bundala Kalolo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea miradi ya umeme mkoani Njombe.
Wajumbe wa bodi,REA,TANESCO na wageni mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa Luponde Hydro uliopo halmashauri ya mji wa Njombe
Mwenyekiti wa bodi hiyo wakili Julius Bundala Kalolo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea miradi ya umeme mkoani Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...