Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuendekeza uongo, fitina, majungu, umbea na kusingiziana ambapo amewakumbusha kuwa, kazi ya siasa ni kusemeana mema, kupendana, kushikamana na kuneneana mema.
Katibu Mkuu ameyasema hayo katika muendelezo wa ziara yake na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Kagera akiwa wilayani Muleba tarehe 14 Novemba, 2021 katika kikao cha shina namba 05 tawi la Lulanda.
Katibu Mkuu amekemea kwa kueleza kuwa, "Kazi ya siasa sio uongo, kazi ya siasa sio majungu, sio fitina, sio umbea wala sio kusingiziana, Kazi ya siasa ni kuombeana mema, kazi ya siasa ni kupendana, kushikamana, kazi ya siasa ni kuneneana mema wenzio."
Kauli hiyo ya Katibu Mkuu imekuja baada ya kupokea taarifa ya viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo walionza kusemana vibaya na kujengeana fitina ikiwa ni maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa ndani ya Chama mapema mwakani.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amezitaka serikali za mikoa na wilaya zinazopakana na ziwa victoria kuendeleza jitihada za kupambana na uvuvi haramu katika ziwa hilo.
Katibu Mkuu amesema, madhara ya uvuvi haramu katika ziwa hilo ni makubwa na kwamba serikali ikiacha kudhibiti matendo hayo, uvuvi haramu utaendelea kutengeneza mazingira magumu kwa mikoa hiyo na wananchi kunufaika na uchumi unaotokana na ziwa hilo.
“Ziwa Victoria ni uchumi mzuri ambao ukilelewa vizuri kwa kufuata uvuvi unaofuta sheria na taratibu, utasaidia kudumu kwa uchumi ambao unatokana na ziwa hilo miaka na miaka,” amesema.
Aidha, wananchi, Madiwani na Wabunge wa Muleba, kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo, wameendelea kutoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali kwa kuwapelekea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa yote ya sekondari wilaya ya Muleba na ujenzi wa vituo vya Afya unaoendelea.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Ndugu Toba Nguvila (kulia) kukagua ujenzi wa madarasa ya shule ya Kabitembe ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja wa Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Kagera ya kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025. ( Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akishiriki ujenzi wa madarasa
ya shule ya Kabitembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali
Charles Mbuge ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja wa Wajumbe wa
Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Kagera ya kukagua,
kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya
2020-2025. ( Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa shina namba 3 Tawi la Kagasha, Kata ya Kabitembe, Muleba ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja wa Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Kagera. ( Picha na CCM Makao Makuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...