Na. Angela Msimbira Kilimanjaro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa Madarasa ifikapo tarehe 15.12.2021
Akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Mhe. Ummy amesema hakutakuwa na uchaguzi wa awamu pili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza (Second Sellection) hivyo ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati ili wanafunzi wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanaanza kusoma kwa wakati mmoja.
Amesema fedha za UVIKO 19 zimetolewa kwa lengo la kuendeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya, na elimu hivyo Viongozi wa Mikoa yote nchini wanawajibu wa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukamilishaji wa ujenzi wa miradi kwa wakati.
Waziri Ummy ametoa maelekezo juu ya kutumia mapaa yenye migongo miwili ili kupunguza gharama za ujenzi na kuhusu matumizi ya vigae amewataka kutumia tarazo au sakafu za kawaida kwa kuwa vigae vinavyowekwa kwenye ujenzi wa madarasa vipo chini ya viwango.
Aidha kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai imepata kiasi cha shilingi milioni 860 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 42.
Ujenzi wa Madarasa ukiendelea katika shule ya sekondari ya Boma , Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akikagua ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari ya Boma, Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro,wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...