MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kazi kubwa ya Serikali ni kujenga mfumo sahihi wa utawala wenye uwezo wa kutengeneza fursa kwa watu wote na kuwawezesha wananchi kuzitumia kwa maslahi yao na taifa kwa jumla.

Mhe. Othman ameyasema hayo jana alipozungumza katika kungamano maalum la kumuenzi aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar marehemu Maalim Seif Sharif Hamad huko hoteli ya Golden Tulip Kiembe samaki mjini Zanzibar.

Aidha amesema pia ni muhimu kuwepo mfumo bora utakaosaidia kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za kiuchumi zilizoandaliwa kwa kuwekeza katika kutengeneza sera bora na usimaimizi wake na kuiwezesha serikali kuwa na uwezo wa kutoa huduma za kiuchumi na kuharakisha maendeleo ya taifa.

Amesema kwamba hatua hiyo itawezesha wananchi kuweza kujiajiri na kuwajiriwa sambamba kuimarisha na kuwepo nyenzo muhimu za kufikia jitihada za pamoja za maendeleo ikiwemo kiwango sahihi cha ukumbwa wa serkikali katika ngazi mbali inayoweza kuwajibika vyema kwa wananchi.

Alisema kwamba kunahaja kubwa hivi sasa Zanzibar kuangalia kwa tathmini ya ukumbwa wa serikali na kufanya mageuzi makubwa ya shughuli zinazofanywa kuanzia ngazi ya serikali za mitaa ambapo kunahitajika kimarishwa kwa kuwa zipo kikatiba.



Amesema kwamba hatua hiyo itasaidia wananchi kurejesha imani kwa serikali yao na kuondosha uhasama na mifarakano inayotokana na sababu za tofauti za kisiasa na hivyo kuendeleza maridhiano ya kweli ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Amefahamisha kwamba haitowezekana kujenga umoja wa kitaifa na maridhiano ya kweli iwapo kama hakujarejeshwa imani ya watu juu ya ushiriki wao katika kuendesha nchi yao kupitia majukwaa ya siasa na uchaguzi katika ngazi mbali mbali.

Amesema kwamba ni lazima kuhakikisha kwamba siasa ni jukwaa sahihi la wananchi katika kuamua hatiuma ya nchi yao kwa kupitia uwanja wa siasa.

Aidha amesema ni muhimu kurejea imani na kuimarisha kuaminiania baina ya mirengu ya viongozi wa kisiasa na wafuasi wao ili wananchi waweze kufahamiana na kuaminia kwa kuwa wakweli.

Amesema kwamba mazingira yanavyojionesha katika serikali ya umoja wa kitaifa hivi sasa ni kuwepo kwa nia njema na utayari wa viongozi jambo ambalo litawezesha kuimarika na kuendelea kujenga umoja miongoni mwa wananchi.

Akizungumza katika Komngamano hilo kuhusu uzoefu wake wa Kumtambua Maalim Seif, rais Msaafu wa awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume alisema kwamba anamtambua Marehem Maalim seif kama ni mtu msahamilivu na mvumilivu aliyeweka mbele masalahi na maendeleo ya wananchi wakati wote.

Amesema kwamba licha ya kuwepo misukosuko kadhaa ya kisiasa katika kipindi kirefu, lakini Maalim Seif hakukata tamaa na wakati wote alipenda kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano ambao ndio jukwa sahihi la kuleta umoja na maridhiano.

Naye Mjane wa Marehem Maalim Seif Mama Awena Sinan Masoud amesema kwamba siri kumbwa ya maalim serif kutokata tama ni kuweka ,mbele dini na dunia katika kuwatumikia wananchi . Amsema maalim seif alitenga vyema muda wake katika kufuatilia miongozo muhimu ya quraan jambo lililomsaidia sana katika kuwa msamehevu na mvumilivu katika masuala na changamoto mbali mbali za kisiasa na kijamii alizokumbana nazo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...