Na Amiri Kilagalila,Njombe

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe limeitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumuondoa kazini ofisa mtendaji wa kijiji cha Ukalawa kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ikiwemo ulevi.

Wakizungumza kwenye kikao cha baraza,madiwani hao wamesema mkurugenzi anapaswa kuchukua hatua za kiutumishi dhidi ya mtendaji huyo ambaye amedaiwa kujihusisha na ulevi wa pombe na kusahau majukumu yake.

“Mtendaji huyu sio kijijiji cha kwanza alikuwa kijiji cha Lupembe ameletwa halmashauri amerudishwa Ukalawa na kote ameenda kuharibu,Mh,mwenyekiti kwenye hili tuangalie sharia zinasemaje,hatuwezi kubaki na hawa watu wanatutesa unampata mtendaji analewa mpaka wananchi wanamshangaa halafu tunaendelea kumbembeleza wa nini?”walisema madiwani

Ofisa Utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi. Sadala Chota amekili mtendaji huyo kuwa ni mlevu ambapo hatua za awali za kiutumishi amesema zilikwisha chukuliwa endapo atarudia hatua za kufukuzwa kazi zitachukuliwa.

“Kweli alikuwa anakunywa sana na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa hiyo malalamiko mengi yalikuja hapa halmashauri,mtumishi huyu alikiri makosa yake na kuahidi kubadirika na tulimuandikia barua ya karipio kali na itakaposhindikana hatua za juu zaidi zitachukuliwa”alisema Bi. Sadala Chota

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Valentino Hongoli amemuagiza mkurugenzi kuchukua hatua za kinidhamu ambapo ametaka mtumishi atakaefanya makosa kwenye maeneo yake hatakiwi kuhamishwa kituo cha kazi kuanzia sasa.


“Mbaya zaidi alikuwa anakunywa wakati wa kazi kwa hiyo tumeazimia kama baraza afunguliwe mashauri ya kinidhamu lakini iwe ni mwisho mtendaji wa kata au wa kijiji amefanya maasi huko halafu arudi”alisema Hongoli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...