Na Mwandishi Wetu - Dodoma
SERIKALI imesema katika miaka ya mwanzoni mwa 1960, Sera za kiuchumi zilijikita zaidi katika uzakishaji na mabadiliko ya kimuundo.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara PROFESA Kitila Mkumbo wakati akizungumza na waandishi wa habari akieleza taarifa ya Maendeleo na mafanikio ya Sekta ya Wizara hiyo katika miaka 60 ya Uhuru.
Profesa Kitila amesema lengo lilikuwa kubadili mfumo wa uchumi wa kikoloni uliojikita zaidi katika viwanda vya uchakataji ( processing industries), kuzalisha bidhaa za kawaida ( Simple Consumer goods) na kuagiza bidhaa muhimu kutoka nje.
Aidha Profesa Kitila amesema hadi sasa Serikali imekamilisha kuvirejesha Serikalini vviwanda ishirini ( 20) na shirika moja kutokana na ukiukwaji wa masharti ya mikataba ya mauzo na pia wawekezaji wake kutoonyesha nia ya kutaka kuviendeleza, Wizara imepata ridhaa ya mamlakae yae kubinafsisha upyae viwanda vilivyokamilika urejeshwaji wake, zoezi la kurejesha viwanda vingine 27 vilivyobaki ambavyo wawekezaji wake wameshindwa kuviendeleza kinaendelea.
Aidha Profesa Kitila amesisitiza kuwa Wizara ya viwanda na Taasisi zake imejipanga na kujizatiti kutekekeza majukumu yake kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye mipango ya kimataifa na bajeti za kila mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...