Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani, Mariam Ulega akizungumza na wapigakura baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kwamba hatawaangusha wanawake wa mkoa wa Pwani. Uchanguzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Pwani Wilaya ya Mkuranga
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
JUKWAA la Wanawake Mkoa wa Pwani wamemchagua, Mariam Ulega kuwa Mwenyekiti wao baada ya kuibuka na ushindi wa kura 29 wapiga walikuwa 41 kura 29 alizizopigiwa zilimpa ushindani wapinzani wake.
Uchaguzi huo umefanyika leo mkoani humo na kabla ya kuwa katika nafasi hiyo Mariam Ulega alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Wilaya ya Mkuranga, nafasi ambayo ameitumikia kwa umakini na weledi mkubwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Mariam Ulega ameahidi kufanya kazi na wanake wote wa Mkoa wa Pwani huku akiwaahidi kutowaangusha wanawake wa Pwani.
"Nitahakikisha nashirikiana wananchi wote wa Mkoa wa Pwani katika kuendelea kuleta maendelo, nitahakikisha nasimama imara katika kufanya kazi na watuote na kuupaisha kimaendeleo mkoa wa Pwani." amesema.
Wakati huo huo Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, leo Novemba 1,2021 ameshiriki uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi la mkoa huo ambapo pia uchaguzi umefanyika kuwapata viongozi wapya na kuwataka viongozi kufanya kazi kwa ari na kasi zaidi ili kumkomboa mwanamke kiuchumi.
"Kimsingi tulikuwa na mabaraza ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kipindi kilichopita. Mwanzilishi wa mabaraza hayo, ni aliyekuwa Makamu wa Rais ambaye kwa sasa ndiye Rais, hapa kati mabaraza hayo hayakuwa na kasi ili iliyokusudiwa." amesema Subira Mgalu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani ,Mariam Ulega (wakwanza kulia)A)akishangilia na wapigakura baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo uchanguzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa mkuu wa Mkoa Pwani.
Wapiga kura wakisubili matokeo baada ya kupiga kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...