Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, ambapo ametoa rai kwa Watanzania wote kushiriki katika zoezi sensa ya watu na makazi mwaka 2022, ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa ufanisi, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiandika maswali ya waandishi wa Habari wakati wa mkutano na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mawasiliano Serikalini, Idara ya Habari MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, akizungumza wakati akihitimisha mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Hayumo pichani,) na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha ya katika miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Hayumo pichani), wakati akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, aliyoitoa katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari wa EATV, Daniel Mkate, akiuliza swali wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Hayumo pichani) wakati akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...