Aliyekuwa katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume (kushoto) akimkabidhi baadhi ya nyaraka za ofisi katibu mpya wa chama hicho wilayani humo Amosi Kusakula baada ya chama hicho kufanya mabadiliko hivi karibuni kwa makatibu wa wilaya na mikoa. Mfaume ameteuliwa kuwa katibu wa CCM wilaya ya Uyui mkoani Tabora
Aliyekuwa katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume (kulia) pamoja na katibu mpya wa chama hicho wilayani humo Amos Kusakula wakipeana maelekezo ya nyaraka mbalimbali wakati wa makabidhiano ya ofisi, Bakari Mfaume anaenda kuwa katibu wa chama hicho katika wilaya ya Uyui wilayani Tabora
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba (aliyesimama) akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa katibu wa chama hicho wilayani humo Bakari Mfaume (wapili kushoto) na katibu mpya wa Amos Kusakula (wapili kulia). Wakwanza kushoto ni katibu siasa na uenezi wa wilaya hiyo Josaya Luoga na wakwanza kulia ni katibu wa wazazi wilayani humo.
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Amos Kusakula(kulia) akisaini baadhi ya nyaraka baada ya kuwasili katika ofisi za chama hicho kwaajili ya kukabidhiwa ofisi na kuanza majukumu yake. Kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM wilayani humo.
Katibu siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Josaya Luoga akisaini nyaraka za kuthibitisha makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa katibu wa chama hicho Bakari Mfaume ambaye anaenda kuwa katibu wa chama hicho wilaya ya Uyui mkoani Tabora na Amos Kusakula ambaye ndiye katibu mpya wa wilaya ya Ludewa.
Aliyekuwa katibu wa wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume (kulia) akimuonyesha mazingira ya nje katibu mpya Amos Kusakula (wapili kushoto) wakati wa makabidhiano ya ofisi. Wakwanza kulia ni katibu wa vijana wilaya Baraka Kalinga na wapili kutoka kulia ni katibu siasa na uenezi wa wilaya hiyo Josaya Luoga
Viongozi wa CCM ngazi ya wilaya wakifurahi wakati wa kumkaribisha katibu mpya wa CCM wilaya ya Ludewa Amos Kusakula (kulia). Kushoto ni katibu siasa na uenezi wa wilaya hiyo Josaya Luoga, aliyekuwa katibu wa CCM wilaya hiyo Bakari Mfaume ambaye anaenda kuwa katibu wa chama hicho wilayani Uyui mkoani Tabora na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba.
Katibu mpya wa CCM wilaya ya Ludewa Amos Kusakula (kulia)akionyeshwa gari ya chama hicho na aliyekuwa katibu wa chama hicho wilayani humo Bakari Mfaume (kushoto) ambaye anaenda kuwa katibu wa chama hicho wilayani Uyui mkoani Tabora
Aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari mfy (kulia) akimuonyesha mipaka ya eneo la chama katibu mpya Amos Kusakula wakati wa makabidhiano ya ofisi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...