Na Abdullatif Yunus Michuzi TV - Kagera.
Halmashauri ya Wilaya Bukoba kupitia mapato yake ya Ndani imetenga Milioni 50 za kumalizia Zahanati na Vifaa Tiba katika Zahanati ya Kansene iliyopo Kata Katerelo Wilayani Bukoba.
Hayo yamebainishwa katika Mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Zahanati hiyo Novemba 11, 2021 wakati ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Murshid Ngeze alipofika Kujionea Maendeleo ya Zahanati hiyo inayojengwa kwa kushirikiana na Nguvu za Wananchi.
Mhe. Ngeze akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukoba Ndg. Fatina Laay pamoja na Mgaga wa Wilaya na Wataalam wengine, amefurahishwa na maamuzi ya Serikali kuridhia kutenga pesa ya kutosha kwa Mara moja ili kukamilisha zahanati hiyo ambayo mpaka Sasa Ina Jengo moja tu, na kusema kuwa maamuzi hayo yataondoa kilio cha siku nyingi kwa wakazi hao ambacho ni kuwasogezea Huduma za Afya karibu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji Bi. Fatina amesema maamuzi ya Halmashauri kutenga kiasi hicho kwa Mara moja kukamilisha Zahanati hiyo kumetokana na namna Wananchi wa Eneo husika kuonesha Nia ya hitajio la Zahanati hiyo, ambapo tayari Wamejitolea Nguvu zao kwa kuchimba mashimo ya Vyoo, wamechanga vifaa vya Ujenzi Mawe na Tofali, hivyo kwa kushirikiana pamoja kutasaidia kuondoa adha mbalimbali za kimatibabu ikiwa ni pamoja na Kupunguza vifo Vya mama na Mtoto.
Aidha kwa Upande Bi Fatina amesisitiza Juu ya Wazazi kuona umuhimu wa Kuwachangia Watoto wao chakula shuleni, kuzingatia Lishe Bora ili kuondokana na utapiamlo pamoja Wananchi kujitokeza kupata chanjo ya Uviko - 19 inayoendelea Sasa maeneo yote na kuwaomba kujitokeza kushiriki zoezi la Sensa hapo mwakani.

Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe Murshid Ngeze akiongea na Wananchi wa Kijiji Kansenene (hawapo pichani) alipofika Kijini hapo kujionea Maendeleo ya Ujenzi wa Zahanati ya Kansenene
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Ndg. Fatina Laay akizungumza na Wananchi (hawapo pichani) wakati walipofika Kansenene kujionea Maendeleo ya Zahanati inayojengwa.
Pichani ni Wananchi wa Kijiji Kansenene wakiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Mhe. Murshid Ngeze wakati akikagua Jengo la Zahanati ya Kansenene inayoendelea kujengwa
Pichani ni Sehemu ya Vifaa vya Ujenzi ambavyo ni mawe na Tofali vilivyokusanywa na nguvu za Wananchi wa Kijiji Kansenene kwa ajili Ujenzi wa Zahanati ya Kansenene.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...