Na Khadija Kalili, Chalinze  
Baada ya kilio cha muda cha ukosefu wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa Chalinze, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) leo imekamilisha utekelezaji wa mradi wa Maji Mlandizi - Chalinze - Mboga utakaondoa changamoto ya muda mrefu ya maji kwa mji mzima wa Chalinze.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji wa Mlandizi - Chalinze - Mboga Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema sasa ni wakati wa Chalinze na maeneo ya karibu kupata maji safi bila kusumbuliwa na kuweza kutimiza lengo la Rais Samia la kumtua Mama ndoo kichwani.

"Leo nimekuja kuwasha mtambo wa kusukuma maji hivyo wananchi wakae mkao wa kula kupata maji safi na salama, Serikali iko tayari kusaidia pale DAWASA inapokwama kwa lengo la kuweza kuwapatia wananchi majisafi na salama.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi unaenda kuondoa kero ya upatikanaji wa Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu unalaza mabomba ya inchi 12 kwa umbali wa Kilomita 59  kutoka mtambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.

Pia amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 18 kimetumika kwenye Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo hivyo kumalizika kwake itakuwa ndio suluhu la upatikanaji wa maji kwenye mji wa Chalinze, Pingo, Pera, Msoga, Bwilingu, Msata, Kihangaiko, na Ubenazimozi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ametoa shukran kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuusimamia na kuhakikisha tatizo la maji Chalinze Wilayani Pwani linakwisha.

"Mkoa wa Pwani ni Mkoa wa kimkakati wa viwanda hivyo ni muhimu kwa wananchi na wawekezaji kuwa na uhakika wa nishati ya  umeme na maji yanayotoka kwa uhakika"alisema RC Kunenge.

Naye Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameishukuru serikali kwa kukamilisha mradi huo maji  unaotekelezwa na DAWASA kwani wanachalinze waliteseka sana.

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakifungua valvu ya maji ili kuruhusu maji kutoka kwenye Mtambo wa kuzalisha majisafi wa Ruvu Juu kuelekea kwenye eneo la Chamakweza, Chalinze ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Maji Mlandizi - Chalinze - Mboga kupitia DAWASA. Wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kuhusu namna uzalishaji wa maji wa Ruvu Juu unavyotekelezwa na DAWASA wakati wa ziara ya kutembelea miradi wa maji pamoja na kungua valvu ya maji ili kuruhusu maji kutoka kwenye Mtambo wa kuzalisha Majisafi wa Ruvu Juu kuelekea kwenye pumpu iliyopo eneo la Chamakwezi ikiwa ni utakelezaji wa mradi wa maji wa Chalinze-Mboga uliotekelezwa na DAWASA wakati wa leo Mkoani Pwani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kuhusu namna uzalishaji wa maji wa Ruvu Juu unavyotekelezwa na DAWASA wakati wa ziara ya kutembelea miradi wa maji pamoja na kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi Chalinze-Mboga uliotekelezwa na DAWASA wakati wa leo Mkoani Pwani.

Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakitebelea Kituo cha kuzalisha maji cha Ruvu Juu wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze- Mboga unaotekelezwa na DAWASA.
Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu uendeshaji wa pampu ya kusukumia maji ya Chamakwezi mara baada ya maji kufika kwenye pampu hiyo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji wa Mlandizi - Chalinze - Mboga unaotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza kulia Meneja wa miradi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Valentina Njau.
Meneja wa miradi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Valentina Njau akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhusu uendeshaji wa pampu ya kusukuma maji ya Msoga. 
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso pamoja, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge pamoja na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwasha Mtambo wa kusukumia maji katika eneo la Mboga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Maji Mlandizi - Chalinze - Mboga kupitia DAWASA.

Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea na kufungua valvu ili kuruhusu maji kutoka kwenye Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu kuelekea eneo la Chalinze, pamoja na kuwasha Mtambo wa kusukuma maji katika eneo la Mboga wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga leo Mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea na kujionea utekelezaji wa mradi wa maji Mlandizi- Chalinze - Mboga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji Mlandizi Chalinze-Mboga uliogharimu sh. Bilioni 18 na uliohusisha kulaza bomba kubwa za inchi 12 kwa Kilometa 59 wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso alipotembelea mradi huo leo Mkoani Pwani.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso kwenye mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga leo Mkoani Pwani
Muonekano wa Pampu ya kusukumia maji iliyopo wa eneo la Mboga Kijiji cha Msoga Mkoani Pwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...