Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amefanya mazungumzo na Bw. Lord Walney, Mjumbe Maalum wa masuala ya Biashara wa Mhe. Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre Dar es SalaaM.

Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kujadili suala zima la kutoa Maji kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma.Pia wamejadiliana masuala mbalimbali kuhusu Utekelezaji wa Miradi ya Maji na changamoto zinazoikumba sekta hiyo hapa nchini.

Serikali ya Uingereza imeonesha utayari wa kufadhili miradi mbalimbali ya maji ikiwemo mradi huo wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma.

Mhandisi Mahundi ameushukuru Ubalozi wa Uingereza kwa kuona jitihada zinazofanywa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata majisafi na salama.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...