Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ambaye pia ni balozi wa bia ya Guinness Smooth, alikuwa kivutio kikubwa kwa wanafunzi wa vyuo mkoani Mbeya ambao walihudhuria uzinduzi wa bia mpya aina ya Guinness Smooth.

Nandy alifanikiwa kuteka mioyo ya wanafunzi walijitikeza kwa wingi katika uzinduzi wa Guinness Smooth ambao walionekana kuwa na kiu kubwa ya brudani ambayo alifanikiwa kuikata

Akiongea katika tukio hilo la uzinduzi, meneja chapa wa SBL Ester Raphael alisema baada ya uzinduzi wa Guinness Smooth bia hiyo sasa itapatikana kwa wingi katika eneo lote la kanda ya Nyanda za juu kusini kwa shilingi 1,500 tu.

Msanii Nandy  akitumbuiza mbele ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa bia mpya ya Guinness Smooth mkoani Mbeya.

Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Denis Tairo akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi aliyejitokeza katika uzinduzi wa bia mpya ya Guinness Smooth jijini Mbeya.


Baadhi ya washindi wa kuimba na kucheza wakiwa wamekabidhiwa zawadi zao katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbali mbali mkoani Mbeya wakiifurahia bia mpya ya Guinness Smooth mara baada ya kuzinduliwa rasmi mkoani humo na eneo zima la kanda ya Nyanda za juu kusini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...