Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 13 Novemba, 2021 amezungumza
kwa njia ya simu na Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina Akinumwi.
Katika mazungumzo hayo,
Dkt. Akinumwi amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jinsi anavyoimarisha sekta
binafsi nchini Tanzania kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Aidha, Dkt. Akinumwi
amemualika Mhe. Rais Samia kuhudhuria Jukwaa La Wawekezaji Afrika,
litakalofanyika nchini Afrika Kusini mwezi Desemba ambalo litatoa fursa ya kuwakutanisha
na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Kwa upande wake Mhe. Rais
Samia amemshukuru Dkt. Adesina Akinumwi kwa
mualiko wenye lengo la kusaidia upatikanaji wa mitaji na uwekezaji wa kimkakati
katika miradi ya maendeleo nchini.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwa njia ya mtandao na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank Group - AfDB) Dkt. Akinwumi A. Adesina leo tarehe 13 Novemba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...