Wa tatu kutoka kulia ni Innocent Simon Moshi -Mkurugenzi mkuu wa Shule ya Lucky Vicent(shari la draft) akiwa na baadhi ya mabalozi wa usalama barabarani katika sehemu iliyojengwa mnara wa kumukumbu ilipotokea ajali wilayani Karatu Mei 6, 2017,na kupoteza uhai wa wanafunzi 32 na waalimu 3
Mkurugenzi Msaidizi Elimu,Habari na Mawasiliano kutoka Rama Msangi akizungumza katika tulio la kuwakumbuka wahanga wa ajali barabaarani ambapo huadhimishwa Kimataifa kila mwaka ambapo RSA walitembelea eneo la rotia ilipotokea ajali ya wanafunzi Karatu.
Augustino Mkumbo,Ni Mratibu wa (RSA)Mabalozi wa Usalama Barabarani kanda ya Mashariki.,akizungumza wakati walipotembelea eneo ulipotokea ajali ya wanafunzi wa shule ya msingi Lucky Vicent wilaya ya Karatu
Mabalozi ww Usalama barabarani RSA wakiwa katika eneo lililojengwa mnara wa kumbukizi ya ajali iliyopoteza wanafunzi takribani wa shule ya lucky vicent iliyopo Jijini Arusha.
Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA )wakiwa katika eneo lililotokea ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 na waalimu 3,ambapo mabalozi hao waliweza kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo la kumbukizi ,Ibada pamoja na kuweka mashada ya maua Kama Ishara ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani ambapo hufanyika kidunia kila ifikapo 24 Nov kila mwaka na kilele chake huwa ni 28 novNa.Vero Ignatus,Arusha
Tukio la ajali ya gari la wanafunzi lililouwa wanafunzi 32 na waalimu 3 katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia,(w)Karatu mkoani Arusha, haliwezi kusahaulika kirahisi mioyoni mwetu,ni historia ambayo haifutiki kizazi hata kizazi,bado tunayo majeraha yasiyotibika:Innocent Simon Moshi -Mkurugenzi mkuu wa Shule ya Lucky Vicent
Katika kuadhimisha Wiki ya wahanga wa ajali duniani ambayo hufanyika 21-28Novemba kila mwaka,yenye kauli mbiu isemayo Kumbuka,Saidia,Tenda, ambapo imeungana na wiki ya nenda kwa usalama barabarani nchini, imeadhimishwa Kitaifa mkoani Arusha "Jali maisha na ya wengine barabarani''
Aidha kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la Afya Duniani, zimekuwa zikieleza kuwa watu takriban milioni 1.35 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, huku wengine kati ya milioni 20-50 wakiachwa na ulemavu kutokana na sababu hiyo hiyo
Tukio hilo la ajali lilitokea Mei 6, 2017, takribani kilomita 150 mji wa Arusha, kilometa 25 kutoka geti la hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ,ambapo Wanafunzi hao walikuwa wamesaliwa na kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea kwaajili ya kujipima kimasomo
Mkurugenzi Msaidizi Elimu,Habari na Mawasiliano kutoka (RSA)Rama Msangi alisema kuwa maadhimisho hayo ya Siku ya wahanga wa ajali duniani (WDoR), yaliasisiwa na Shirikisho la Vyama vya Wahanga wa Ajali za Barabarani, huko barani Ulaya, mwaka 1995 ambapo miaka 10 baadae, mwaka 2005, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilitangaza kuchukua jukumu la kufanya maadhimisho haya na kupitia Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye namba 60/5.
Msangi alisema kuwa kwa mabalozi hao mkutembelea eneo hilo lilitokea ajali,wanakuwa wamegusa sehemu ya tatu ya dhima hiyo, ambayo ni kuchukua hatua,ya kuwafanya wahusika kuchukua hatua za kuboresha miundombinu ya eneo hilo ilipotokea ajali ,hiyo
wametimiza sehemu ya kwanza ya maadhimisho ya mwaka huu, ambayo ni kuwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki zetu waliopoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.
Aidha Sehemu nyingine ya dhima ya mwaka huu, inawataka kuwapa sapoti wale waliopata madhara ya ajali kwa ukubwa mbalimbali "Tusiwatenge kwasababu bado ni wenzetu. Mke asiache kume kisa amekuwa mlemavu baada ya ajali, mume pia asiache mke kwasababu hizo hizo.Alisema Msangi''
Augustino Mkumbo,ni Mratibu wa (RSA)Mabalozi wa Usalama Barabarani kanda ya Mashariki., alisisitiza kuwa msukumo wa kuchukua hatua kama zinazofanywa na RSA Tanzania za kuelimisha kuhusu umuhimu wa kila mmoja kuhakilisha kuwa usalama barabarani unaimarika katika pande zote.
Lakini kubwa zaidi kuwapa sapoti vijana na watoto wetu waliopata madhara ya ajali ,kwa kuwawekea mazingira ya kuendelea kutengeneza njia za kutimiza ndoto zao,"tusiwaachishe shule kwa wale wanaosoma, tuwape vifaa vitakavyorahisisha usomaji wao''.alisema Mkumbo''
Akizungumza mkurugenzi wa Lucky Vincent Innocent Simon Moshi, kuwa tukio hilo haliwezi kusahaulika kirahisi ,ni historia amabayo haitasahaulika kizazi hata kizazi mioyoni mwao,kwani watoto wadogo ambao wangekuja kulitumikia taifa la Tanzania walipoteza maisha katika ajali ya barabarani pamoja na kupoteza nguvukazi ya taifa waalimu
''Tulipatwa simanzi kubwa sana mioyoni mwetu na mpaka sasa simanzi hiyo inaendeleasio suala jepesi tunalolizungumza,lakini sikuile kwa wale waliobahatika kufika na kuona hakukuwa na alama yeyote ya kuasiria harai, halikuwa jambo jepesi kabisa lilikuwa ni suala zito,lakini tunashukuru sana kwa faraja mpaka leo tumeweza kufikia hapa''
Katika kumbukizi Ajali hii ya gari la wanafunzi shule ya Lucky Vincent,iliyopo,ilitokea kaskazini mwa Tanzania,linaonekana likiwa limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia,(w)Karatu mkoani Arusha Mei 6, 2017 ambapo ni takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro , kilomita 150 kutoka mji wa Arusha,ambapo wanafunzi hao walikuwa wamesalia na kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea kujipima kimasomo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...