Na Khadija Kalili , Kibaha
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Watu Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga amesema serikali imekopesha watu wenye ulemavu kiasi cha. Bil.12.9 hadi kufikia Agosti mwaka huu fedha zitokanazo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashaur zote nchini.
Mheshimiwa Nderiananga alisema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe yaliyofanyika kitaifa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani ambapo alisema kuwa fedha hizo zimeweza kuwanufaisha kama jinsi ilivyolengwa watu hao wenye ulemavu.
"Watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa kama walivyo watu wanaoona na wanauwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi" alisema Nderiananga.
Wakati huohuo Naibu Waziri huyo ametoa wito kwa watu wenye mahitaji Maalumu kujitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi la kuhesabiwa sensa wakati utakapofika kwani itasaidia serikali kujua idadi yao kamili Ili waweze kuona namna ya kusaidiwa katika nyanja mbalimbali.
Mkurugenzi wa Elimu anayeshughulikia watu wenye mahitaji maalumu kutoka Wizara hiyo Margareth Matonya alisema kuwa mwaka huu wametoa mafunzo kwa walimu na 1,373 wathibiti ubora 200 kwa lengo la kukagua miundombinu kama inafikika eneo la ufundishaji na wanaangalia walimu wanavyofundisha wanafunzi wenye ulemavu kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani alisema kuwa mkoa huo umejenga mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye Halmashauri mbili ambazo ni Chalinze na Mkuranga.
Awali mwenyekiti wa Chama Cha Wasioona TLB Omary Sultan alisema kuwa maadhimisho hayo ni kwa ajili ya kukaa na kutafakari masuala mbalimbali ya wanachama ili kujua changamoto na mafanikio na kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, afya na masuala ya maendeleo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Watu Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga
Naibu Waziri Nderiananga akiimba na kucheka na bendi ya Ruvu iliyotumbuiza kwenye maa dhimisho a Fimbo Nyeupe ,Mwenye Koti la buluu ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri
Mwenye miwani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wasioona Taifa Omary Sultan
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...