Na Josephine Majura, WFM, Dar es Salaam
Serikali
imetoa wito kwa Washiriki waliohusika na utoaji wa elimu kwa Umma
katika Maadhimisho ya kwanza ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kuendelea
kutoa elimu ili kuwezesha watanzania wengi zaidi kuwa na uelewa wa
masuala ya elimu ya fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Wito
huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji
Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba wakati akifunga Maadhimisho ya Wiki
ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
“Naomba tuendelee kushirikiana na
wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha katika kuhakikisha malengo ya
Maadhimisho haya yanafikiwa hususan kwa watu ambao kwa namna moja au
nyingine hawakupata fursa ya kuhudhuria maadhimisho haya alisema Bw.
Tutuba”.
Aidha Bw. Tutuba alisema kuwa ili kuhakikisha elimu
inawafikia wananchi wote Serikali kupitia wizara hiyo imeandaa utaratibu
wa kutoa elimu kwa njia ya makundi ambapo itakua na Siku ya Elimu ya
Fedha kwa Watoto, Wanawake, Vijana na Wajasiriamali Wadogo pamoja na
Elimu ya Fedha kwa Viongozi wa Kisiasa katika ngazi mbalimbali,
Wahariri, Wastaafu na wengineo.
Alifongeza kuwa Serikali
itaendelea kuwekeza katika Sekta ya Fedha na kuendelea kufanyia kazi
changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ikiwemo masuala ya riba katika
mabenki kuhakikisha zinakua rafiki kwa wananchi ili waweze kunufaika na
sekta hiyo ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi na Taifa kwa ujumla.
Bw.
Tutuba alimshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wizara ya Fedha na
Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, ambaye alifungua Maadhimisho ya
Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa siku ya Jumatano, tarehe 10, Novemba
2021 na kuwashukuru wote waliohudhuria maadhimisho hayo pamoja na Timu
ya Wataalam iliyofanya maandalizi na kuwezesha kufanyika kwa maadhimisho
hayo.
Kwa upande wake Kamishna wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha
nchini Dkt. Charles Mwamwaja, alisema kuwa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma
Ndogo za Fedha Kitaifa yamefanyika ikiwa ni utekelezaji wa Programu
yake ya Uelimishaji Umma ya Miaka mitano (National Financial Education
Programme; 2020/21-2025/26).
Aliongeza kuwa wizara itaendelea
kutoa elimu ya masuala ya fedha kwa umma ili kuongeza uelewa na weledi
kwa umma kuhusu huduma za fedha zinazotolewa ili kujenga uchumi na
kuondoa umasikini.
Kwa upande wao washiriki wa maadhimisho hayo
ikiwemo Benki, Taasisi za Bima, Masoko ya Mitaji na Dhamana, Mifuko ya
Jamii na Huduma ndogo ya Fedha, wameipongeza wizara kwa kuandaa
maadhimisho hayo kwa kuwa wameweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo
yatasaidia kukuza sekta hiyo.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yaliyofanyika kwa siku saba katika viwanja vya
mnazi mmoja jijini Dar es Salaam yamekamilika leo, ambapo maadhimisho
mengine yanatarajiwa kufanyika mwakani mwezi Novemba.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza
wakati wa kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa
yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam,
ambapo amewataka wataalamu wa masuala ya fedha kuendelea kutoa elimu kwa
Umma.
Kamishna
wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Charles Mwamwaja akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Wiki
ya Huduma za Fedha Kitaifa, Maadhimisho hayo yamefungwa na Katibu mkuu,
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza
jambo alipotembelea banda la Benki ya TIB, wakati wa kufunga Maadhimisho
ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko na Masuala ya
Biashara wa Benki ya TIB, Bw. Said Mkabakuli..
Katibu
Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akifurahia jambo
na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha
na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja baada ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya
Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mkuu wa Tathmini ya Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw.
George Nyamrunda akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba,
alipotembelea banda hilo wakati wa kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Huduma
za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (Katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya
Huduma za Fedha Kitaifa. Kulia waliokaa ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar
es Salaam, Bw. Hassan Rwaga, kulia kwa Katibu Mkuu ni Kamishna wa Idara
ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Charles Mwamwaja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...