Serikali imefuta matokeo ya nadharia (theory) kwa masomo ya program ya Utabibu Ngazi ya Tano (NTA Level 5) baada ya kubainika kuvuja kwa mitihani ya muhula wa pili wa programu hiyo.

Akitangaza maamuzi hayo jijini Dodoma, leo Novemba 4, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichalwe amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa kuchunguza viashiria vya uvujifu wa mitihani hiyo iliyofanyika ilifanyika 16 Agosti, 2021 hadi 30 Septemba, 2021.

“Wakati wa uchunguzi wa mitihani iliyovuja, kamati ilibaini kuwa mitihani hiyo ilisambazwa kupitia mitandao ya kijamii (telegram na WhatsApp) na kuonekena kwenye baadhi ya namba za simu za wanafunzi zilizofanyiwa uchunguzi na kamati.

Kupitia sheria ya Baraza Sura 129 na Kanuni za Mitihani, Kifungu 33 (1) (iii), 2004 limefuta matokeo ya mitihani ya nadharia (theory) kwa masomo yote ya Programu ya Utabibu Ngazi ya Tano na baraza limeagiza kurudiwa kwa mitihani hiyo upya ndani ya wiki Sita kuanzia tarehe Novemba 1, 2021.” Amesema Dk Sichalwe.

Mganga Mkuu huyo pia amesema mitihani hiyo itafanyika sambamba na mitihani ya marudio (supplementary Exams) kwa program zingine za afya nchi nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...