SERIKALI imepiga marufuku kusafirisha malighafi ya mazao ya misitu kwenda nchi za nje

Akitangaza marufuku hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema yeyote atakayebainika kusafirisha mazao hayo ya misitu atafutiwa leseni ya kusafrisha mazao hayo

Ameyataja mazao hayo kuwa ni magogo ya miti, gundi inayogemwa kwenye miti aina ya misindano pamoja na ''timber veneer''

Dkt. Ndumbaro amewataka wenye viwanda kuchakata mazao hayo kwa kuyaongezea thamani hadi hatua za mwisho hapa nhini ili kuwanufaisha Watanzania kwa kupata ajira kwenye viwanda

Ameyasema hayo kweye kongamano la Uwekezaji wa Sekta ya Misitu mkoa wa Iringa ambalo limefanyika kwa muda wa siku mjini Mafinga na kuwakutanisha Wabobezi wa masuala ya misitu wa ndani na nje ya nchi pamoja na wadau wa misitu kujadili changamoto na fursa zilizopo katika zao hilo.

Akizungumzia marufuku hiyo, Dkt. Ndumbaro amesema maono ya serikali kwa sasa ni kuendeleza viwanda hivyo haiwezekani mazao ya misitu yakendelea kusafirisha kwenda nchi za nje huku Watanzania wakibaki watzamaji tu

'' Tanzania ya viwanda haitaweza kufanikiwa kama Mimi Waziri mwenye dhamana nitaruhusu malighafi ya mazao ya misitu zitaendelea kusafrishwa kwenda nchi za nje sasa viwanda vyetu vitakua vipi '' alihoji Dkt. Ndumbaro

Wakati huo huo, Dkt. Ndumbaro amepiga marufuku biashara ya gundi inayogemwa kwenye miti aina ya misindano hadi pale maamuzi mengine yatakapotolewa

Kufuatia marufuku hiyo, Dkt.Ndumbaro ametoa muda wa siku 30 kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kuwasilisha ripoti juu ya faida na athari za ugemaji gundi hiyo

Akitoa msimamo huo, Dkt.Ndumbaro amewataka wenye uhitaji wa gundi hiyo wafungue viwanda nchini na sio kusafirisha malghafi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...