TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imevamiwami kambini jijini Antananarivo na Kundi la Wanajeshi wa nchi ya Madagascar wakidai wakuwafuata baadhi ya Wachezaji wa timu hiyo ambao wanadai wana maambukizi ya COVID-19, baada ya hapo kutoka kwa taarifa hizo wakati timu hiyo ilipotua nchini humo.
Taifa Stars imetua nchini humo kwa ajili ya mchezo wake wa mzunguko wa mwisho wa Kundi J, mchezo ambao utachezwa leo siku ya Jumapili katika dimba la Manispaa ya Mahamasina uliopo jijini Antananarivo nchini humo.
Tayari taarifa hizo zimeripotiwa na baadhi ya wadau wa Soka walioambatana na Timu hiyo ya Tanzania akiwemo pia Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Clifford Ndimbo. Madagascar wanadai Wachezaji Mbwana Samatta, Kipa Aishi Manula na Beki Bakari Mwamnyeto wana maambukizi ya COVID-19.
Akizungumza na Kituo cha Runinga cha Azam TV, Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani amesema waliomba kupimwa tena kwa Wachezaji hao (Retest) na wakakutwa hawana maambukizi ya COVID-19 (Negative), vipimo hivyo vya mara ya pili vikishuhudiwa na jopo la Madaktari wa Taifa Stars, Wataalamu wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) na baadhi ya Wataalamu wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...