Na. John Mapepele, WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe.
Innocent Bashungwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
Filamu nchini inatarajia kwa mara ya kwanza tangu Tanzania kupata uhuru wake kufanya
tamasha kubwa la kihistoria la utoaji wa tuzo mbalimbali za filamu ambalo
litafanyika Disemba 18, 2021 jijini Mbeya.
Akizungumza na kwenye Mkutano wa Waandishi wa
habari jijini Mbeya, Novemba 29, 2021 Mhe. Bashungwa amesema sababu kubwa ya
kufanyia kilele cha tuzo hizi jijini Mbeya ni kutambua uwepo wa wanatasnia ya
filamu pamoja na wasanii katika mikoa na maeneo mengine nje ya Dar es Salaam ili
kuamsha ari ya kufanya kazi za sanaa na hatimaye kujipatia ajira na kipato
kitakacho boresha maisha yao.
“Tamasha
hili linakwenda kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko maeneo hayo katika
uwanja huu wa filamu na Sanaa kwa ujumla kupitia idadi kubwa ya wapenzi wa
filamu watakaokuwa wanafuatilia tukio hili ndani na ncje ya nchi yetu.”.
Amefafanua
Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.
Samia Suluhu Hassan, imedhamilia kuleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya
sanaa na Filamu ndyo maana imekuwa na miokakati mbalimbali ya kuboresha tasnia
hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa tuzo za
filamu kwa wanatasnia ya filamu hapa nchini kwa lengo la kutambua mchango wa
wahatasnia hao.
“Kwa mwaka huu wa fedha, Mhe. Rais ametenga kiasi
cha Sh. Bilioni 1.5 kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni
ambao niliuzindua tarehe 22 Novemba 2021. Mfuko huo utatoa mikopo na kuwezesha programu
mbalimbali za kuendeleza Sanaa nchini ikiwemo filamu” amefafanua Mhe. Bashungwa
Akifafanua zaidi
Mhe. Bashungwa amesema katika kuboresha
kazi za sanaa na Filamu nchini Novemba 22, 2021, alizindua Mfumo wa kidijitali utakaokuwa unatumiwa na
Taasisi za BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA, ambazo ziko chini ya Wizara yake.
Ametaja baadhi ya faida
za mifumo hiyo kuwa ni pamoja na kurahisha utendaji wa Taasisi hizo katika kuwahudumia
wasanii kwa kutia huduma kwa haraka,kuwarahisishia wasanii wote nchini na hata
nje ya nchi kupata huduma kokote walipo bila kufika katika ofisi hizo, ambazo
ni BASATA, BODI YA FILAMU na COSOTA na kutunza kumbukumbu za wasanii na kuleta wepesi
wa kuwatambua kokote walipo ili kurahisisha utoaji huduma kwao kama vile mafunzo
mbalimbali ya Sanaa ambayo Taasisi hizi zimekuwa zikiyatoa.
“Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha nguvu na mchango
mkubwa wa Tasnia ya Filamu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi. Sekta ya burudani
inayohusisha filamu imefanya vizuri katika nyanja za Kiuchumi, kwa mfano, mnamo
mwaka 2018 Sekta hii iliongoza kwa ukuaji wa kasi ya zaidi ya 13%, ambapo ilishika
nafasi ya tatu mwaka 2019 kwa ukuaji wa kasi ya 11%. “ amesisitiza Mhe. Bashungwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...