NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ameeleza kuwa taratibu za urasimishaji wa biashara nchini kwa kusajili na kutoa Leseni za biashara na viwanda kwa njia ya mtandao kupitia BRELA zimesaidia kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuwezesha nchi kuwa katika kiwango bora cha ufanyaji biashara duniani.

Mhe. Kigahe ameeleza hayo Novemba 08, 2021 katika kikao cha mafunzo kwa Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania kuhusu makapuni na majina ya biashara; leseni za biashara na za viwanda; na miliki ya ubunifu   yaliyotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma.

Mhe. Kigahe amebainisha kuwa utoaji huduma za BRELA kwa njia ya mtandao umepunguza sana na kudhibiti vishoka waliowasumbua wateja wakati walipohitaji huduma kama kusajili makampuni na majina ya biashara.

Aidha, Mhe. Kigahe ameeleza kuwa kupitia utekeleza wa Blueprint watapitia  baadhi ada na tozo zinazotozwa na BRELA kwa kuziondoa au kuzipunguza ili Watanzania waweze kurasimisha biashara zao vilevile baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba wateja kwenye mtandao zimetatuliwa na wanaendelea kufanyia maboresho Zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni BRELA, Bw. Andrew Mkapa wakati akitoa mafunzo juu ya usajili wa makampuni na majina ya biashara amefafanua kuwa baadhi ya wateja wamekuwa wakishidwa  kutofautisha kati ya kampuni na jina la biashara  huku akieleza kisheria ni vitu viwili tofauti.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...