Khadija Kalili, Mafia
Timu ya Nyika FC ya Kibaha imeibuka mshindi katika fainali za michuano ya Ligi Mabingwa Mkoa wa Pwani kwa kuichapa Kerege FC bao mbili kwa nunge.
Kufuatia ushindi huo Nyika FC watacheza na Mabingwa kutoka katika Mkoa mingine kwenye michuano ya RCL .
Nyika FC ilikutana na vijana wa Kerege wenye maskani yao Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika mechi iliyochezwa jana jioni katika Uwanja wa Dawindege Kilindoni Wilayani Mafia Mkoa wa Pwani.
Mchuano huo ulikuwa mkali ambapo pande zote walicheza kwa kukamian kuwania nafasi hiyo ambapo mwanzo wa mchezo hadi mwisho wachezaji wa Kerege FC waliumudu mpira ipasavyo lakini bahati ya kuzitikisa nyavu za timu ya Nyika FC haikuwa yao hali iliyowafanya vijana wa Kerege kutoka vichwa chini
hadi kipenga cha mwisho kilipopigwa na aliyekuwa Mwamuzi wa mechi hiyo Ally Mangunga.
Kwa ushindi huo Nyika FC watacheza Ligi Daraja la tatu huku michuano hiyo ikiwa imeandaliwa na Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA)
Akizungumza na Michuzi Blog baada ya mechi Kapteni wa timu ya Kerege FC Chande Makoja alisema kuwa yeye na wenzake walicheza Ili waweze kupata ubingwa lakini bahati haikuwa kwao wanamshukuru Mungu kwa yote.
Wakati
huohuo Meneja wa Timu ya Kerege FC Nassir Mohammed amelalamikia namna
mchezo mzima ulivyochezeshwa pamoja na matokeo ya mechi hiyo huku
akilalamika ubovu wa kiwanja ambacho mechi hiyo ilichezwa huku
akilalamika kuwa Kerege FC waliandaliwa hujuma ya kukwamishwa lakini
waliingia Uwanjani huku wakiwa tayari wakijua wanakwenda kuang'olewa
lakini waliamua kutimiza wajibu wao wa kucheza.
Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira Mkoa wa Pwani (COREFA) Ibrahim Gama aliyekuwepo mwanzo hadi mwisho wa mechi hiyo alisema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa uongozi wa Kerege FC na kuwataka wafuate taratibu ya kutoa vithibitisho dhidi ya tuhuma hizo na COREFA watachunguza na haki itatendeka .




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...