Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa kasi na kufikia zaidi ya asilimia 8 katika kipindi Cha miaka mitano ijayo
Matarajio hayo yanatokana na kuongezeka kwa Matumizi ya rasilimali na ongezeko la tija katika shughuli za uzalishaji.
Akifungua Mkutano wa 20 wa Taasisi za fedha nchini uliofanyika leo November 25, 2021 Jijini Dodoma, Gavana wa Benki Kuu Tanzania Profesa florens Luoga amesema ili kusaidia hilo wanatekeleza hatua za kisera ikiwemo zinazolenga kupunguza riba za mikopo na kuongeza ukwasi katika mabenki.
Amesema kwa sasa wanahakikisha mfumuko wa bei nchini unakuwa wa kiwango cha chini,thamani ya Shilingi dhidi ya Fedha za kigeni inaendelea kuwa imara ili kuongeza mikopo kwa Sekta binafsi na kuchangia ukuaji wa uchumi.
"Tanzania pia itaendelea na maandalizi ya kununua dhahabu yenye ubora unaotakiwa kutoka viwanda vya kusafisha dhahabu vilivyopo nchini,"alisema.
Profesa Luoga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muunganano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake alizofanya kuhusiana na fedha za IFM kwa ajili ya kushughulikia changamoto UVICO19.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...