MWENYEKITI wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema maambukizi ya UVIKO-19 yameendelea kuathiri shughuli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwani makongamano, tafiti na ubunifu na shughuli nyingine zinazohusisha mikusanyiko ya watu zilifanyika kwa tahadhari kubwa.
Ameyasema hayo wakati Mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
Prof Anganisye amesema UVIKO-19 umeathiri kwa kiasi kikubwa mchakato wa ununuzi wa vifaa vya ujifunzaji na ufundishaji na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo.
Pamoja na hayo amesema wanafunzi wapatao 1,565 watahitimu na kutunukiwa digrii na Stashahada mbalimbali katika kitivo cha Sayansi za Jamii, Kitivo cha Elimu na Kitivo cha Sayansi.
Aidha Prof.Anangisye amesema katika mwaka wa masomo 2020/2021, Chuo kimeanzisha ushirikiano na Taasisi 5 za Kimataifa katika nyanja mbalimbali hasa tafiti, utoaji wa mafunzo na ubadilishanaji wa ujuzi na maarifa.
“Wahitimu wanafahamu kuwa ingawa wao ndio waliokaa darasani, kwenda maktaba na kufanya utafiti, mafanikio yao yametokana na michango ya wadau wengi ikiwa ni pamoja na Serikali,familia, asasi na watu mbalimbali”. Amesema
Kwa Upande wake Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.Stephen Maluka amesema kwa mwaka 2020/2021 Chuo kilitenga Shilingi Milioni 413.5 kwaajili ya mafunzo ya watumishi kati ya kiasi hicho, shilingi milioni 113.5 ni kwaajili ya mafunzo ya muda mfupi na shilingi Milioni 300 kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu.
Amesema Chuo kilitenga shilingi Milioni 300 katika bajeti ya mwaka 2020/2021 kiasi ambacho kinatarajiwa kuongezeka kila mwaka kadri itakavyowezekana.
“Shughuli za kiutafiti zimeenda sambamba na kuongezeka kwa machapisho yanayotolewa na wanataaluma wa Chuo. Ili kuimarisha shughuli za kitafiti, jarida la Chuo liitwalo Journal Of Education, Humanities and sciences, ambalo lilipata hadhi ya Kimataifa mwaka 2017 limeendelea kuchapishwa kwa wakati na hivyo kuwavutia wanataaluma wengi ndani na nje ya nchi kuchapisha matokeo ya tafiti “. Amesema Prof.Maluka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof.Stephen Maluka akizungumza wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam wakifurahi wakati wa mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...