Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Rejareja wa Benki ya Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere (kulia), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo, Robert Lowassa, mara baada ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya Afya ya wateja maalumu wa Benki ya Absa ambayo kupitia klabu hiyo wateja, familia zao na wafanyakazi wa Absa watapata huduma za Afya ya mwili na akili bila gharama kutoka kwa washirika wa Absa. Huduma hizo ni pamoja na ushauri na upimaji wa Afya, mazoezi ya viungo na elimu ya lishe. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam Jana.
kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere akizungumza na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Afya ya wateja maalumu wa Benki ya Absa ambayo kupitia klabu hiyo wateja, familia zao na wafanyakazi wa Absa watapata huduma za afya ya mwili na akili bila gharama kutoka kwa baadhi ya washirika wa Absa na wengine kwa punguzo la bei. Huduma hizo ni pamoja na ushauri na upimaji wa afya, mazoezi ya viungo na elimu ya lishe. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam Jana
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakifanya mazoezi ya yoga yakitolewa na mtaalamu kutoka Mukti, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya Afya ya wateja maalumu wa Benki ya Absa ambayo kupitia klabu hiyo wateja, familia zao na wafanyakazi wa Absa watapata huduma za afya ya mwili na akili bila gharama kutoka kwa baadhi ya washirika wa Absa na wengine kwa punguzo ya bei. Huduma hizo ni pamoja na ushauri na upimaji wa afya, mazoezi ya viungo na elimu ya lishe. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam Jana.
Uzinduzi wa Absa Bank health club uliyanguliwa na mbio za kilomita tano na kumi za kujifurahisha. Pichani baadhi ya washiriki wakichuana vikali ili kumaliza mbio hizo katika mitaa ya Masaki, Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Absa wakishiriki mbio za kilomita 10 kuashiria Uzinduzi wa Klabu ya Afya ya benki hiyo kwa wateja maalum jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Absa wakipasha viungo kabla ya kuanza kwa mbio za kilomita tano na 10 zikiwa sehemu ya shamra shamra za uzinduzi wa Klabu ya Afya ya benki hiyo kwa wateja maalum jijini Dar es Salaam jana. Mtaalamu wa mazoezi ya viungo kutoka Pure Fitness aliongoza kipindi hicho.
Meneja wa Kituo cha Wateja Maalumu wa Benki ya Absa, Agnes Paul Mushi (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wao, Namwaka Omary Mara baada ya uzinduzi wa Absa health club jijini Dar es Salaam jana.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...