VIJANA nchini wameshauriwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika sekta ya michezo hasa katika mpira wa miguu.
Rai hiyo ameitoa Mbunge wa Jimbo la Welezo Mhe.Maulid Saleh Ali wakati akikagua matengenezo ya uwanja wa mpira wa Matemwe ulipo katika Jimbo hilo.
Amesema kuwa michezo kwa sasa ni miongoni mwa sekta inayotoa ajira nyingi kwa vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali kujipatia fedha
Aliwambia vijana hao waendelee kutumia vizuri uwanja huo kwa kufanya mazoezi na kushindana na timu mbalimbali za majimbo jirani ili wapatikane wachezaji wenye vipaji na uwezo mzuri wa kucheza mpira.
Amewaahidi vijana hao kuwa ataendelea kuwaunga mkono katika masuala mbalimbali yakiwemo ya michezo ili kwenda sambamba na matakwa ya Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Alieleza kwamba ametoa vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na kudhamini ligi za jimbo hilo za vijana pamoja na kuibua vipaji vya vijana wadogo ambao kwa sasa wana uwezo mzuri wa kucheza mpira na michezo mingine.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa Jimbo hilo Ayoub Saleh Ayoub, alisema uwanja huo ulikuwa na umeanza kuharibiwa na maji ya mvua hivyo wanaufanyia matengenezo ili vijana wapate uwanja wenye viwango.
Aidha alisema mbunge huyo amekuwa akijitolea kufanikisha masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo hivyo amewasihi viongozi wengine kuiga mfano huo wa kiutendaji.
Kwa upande wake Farid Juma Issa ambaye ni miongoni mwa vijana wanaotumia uwanja huo, alimpongeza mbunge huyo kwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kutengeneza uwanja huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...