Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Arusha
WATUMIAJI wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kutii sheria bila shuruti ili kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipoteza nguvu kazi nyingi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kimataifa ya uuzaji wa magari ya BE FORWARD yenye makao yake makuu jijini Dar es Saalam,Daniel Japhet wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda lao katika uwanja wa Stadium jijini Arusha.
Amesema kuwa,endapo watumiaji wa barabara watatii sheria bila shuruti itapunguza Sana ajali zinazoweza kuepukika.
“Sisi kama wadau wa kuuza magari Tanzania tunahamasisha watumiaji kutii sheria na kufuatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuzitumia bidhaa zetu kwani zina ubora wa hali ya juu na huo ndo ukweli na uwazi sisi hatuna biashara ya longolongo tunajiamini kwa kile tunachokifanya,"amesema Daniel.
Amesema wao kama wauzaji wa magari Tanzania wameona watoe sehemu ya faida yao kwa ajili ya kuja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto katika kuwahamasisha kufuatia sheria na kanuni ili kuepukika kwa ajali.
“Tumekuwa tukitengeneza wastani wa magari elfu nane hadi elfu kumi kwa mwezi ambapo tumekuwa tukitumia bandari ya Dar es Saalamu Zambia na Malawi, hivyo tunawaomba Sana wananchi wajitokeze kwa wingi kutuunga mkono kwa kununua bidhaa zetu kwani ni za uhakika na Zina ubora wa hali ya juu,”amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wamiliki wa malori wadogo na wa kati,(TAMSTOA)Chuki Shabani amesema kuwa chama hicho kipo Kama ngazi kati ya Serikali na wanachama katika kushirikiana kutoa elimu kwa wafanyabiashara wasafirishaji wa malori juu ya umuhimu wao katika kufuata sheria .
Amesema kuwa, madereva malori wamekuwa wakisoma mara kwa mara kwa ajili ya kujikumbusha jinsi ya kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani na kuepukana na ajali za mara kwa mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...