KAMPUNI ya Wavesleek kupitia Mtandao wao wa Seto wameamua kuja na suluhisho kwa ajili ya wapangaji wa nyumbani na hoteli kupitia huduma ya kiganjani kwa bei nafuu ambapo sasa huduma hiyo itarahisisha upatikanaji makazi,hoteli na sehemu za biashara kwa haraka

Akizungumza leo Novemba 29,2021, Mmiliki wa Kampuni ya Wavesleek Hamza Jabir amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto  wanazopata watu wanaotafuta makazi pamoja na sehemu za biashara wameona iko haja ya kutambulisha rasmi huduma ya Mtandao mpya wa Seto itakayosaidia upatikanaji wa nyuma za makazi na maeneo ya biashara kwa haraka bila usumbufu wowote.

"Mtandao huu unalenga kurahisisha upatikanaji wa Nyumba, sehemu za biashara,  kupitia Mtandao wa Setto Kwa kupakua na kujisajiri na malipo  yake ni Sh.10,000," amesema na kufafanua kumekuwa na changamoto nyingi mtu anapohitaji makazi au eneo la biashara,hivyo wamekuja na suluhu.

Amesema kumekuwa na mzunguko mrefu na wenye usumbufu, kwani ilikuwa lazima mhusika atagute dalali  na kumpatia fedha kwa ajili ya kumtafutia makazi au eneo la biashara."Hivyo basi kuwepo kwa Mtandao huo wa SETO utakusuluhisho na kumaliza changamoto hizo".

Jabir ameongeza kwa vijana ambao wamekosa ajira kwa kupitia huduma hiyo ya Mtandao huo Seto wataweza kujipatia ajira kwa urahisi kama Madalali.

" Nawaomba vijana wakimbilie fursa hiyo ya udalali kupitia Mtandao wa Seto kwa kusambaza picha za nyumba ambazo zinapangishwa au kuuzwa,kwa kufanya hivyo wataweza kupata Sh.6000 kama malipo yao.

Mmiliki wa Kampuni ya Wavesleek Hamza Jabir akizungumza na waandishi Wahabari mara baada ya kuzindua  Mtandao wa "Seto" wenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa Nyumba, sehemu za biashara Kwa wanaohitaji kupanga kupitia simu zao za Viganjani.

Baadhi ya wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi wa Huduma ya kimtandao "Seto'' ya upatikanaji wa Nyumba, sehemu za biashara Kwa njia ya kiganjani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...