Jane Edward,Arusha

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amezitaka nchi za Afrika Mashariki kuwekeza zaidi kwa  vijana ili kuharakisha maendeleo ya haraka katika kukuza uchumi wa nchi na bara la Afrika kwa ujumla.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akizindua Jukwaa la usawa wa kijinsia  kwa vijana programu ya YouLead Afrika mashariki katika kituo cha kimataifa cha maendeleo ya jamii na utawala bora MS TCDC Mkoani Arusha

Amesema Mkutano huo wa tano wa Vijana wa Jumuiya hiyo ni muendelezo wa jitihada za nchi za jumuiya na Afrika kutengeneza vijana viongozi wa kesho ingawa bado changamoto za ukosefu wa ajira bado ni tatizo.

"Kauli mbiu ya jukwaa la vijana 2021 ni kutengeneza mustakabali wa ajira kwa vijana Afrika na duniani kwa ujumla lakini pia kuwezesha mtoto wa kike kupata fursa mbalimbali kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia"Alisema Majaliwa

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO mwaka 2020 takwimu zinaonyesha kuwa  asilimia 6.8 nchi za Afrika zinakabiliwa na ukosefu wa ajira hali inayosababisha nchi hizo ikiwemo Tanzania kuja na dira mbalimbali za kukabiliana na ukosefu wa ajira .

Amebainisha kuwa kwa sasa nchi za Afrika hazina budi kutengeneza ajira ili waweze kujikita katika kukuza uchumi na kuendana na kasi ya dunia hasa katika nyanja za kilimo,Madini,ufugaji .

"Katika kipindi hiki wenzetu wanatembea sisi tunatakiwa kukimbia ili kuweza kukuza uchumi wetu ambapo kwa kasi hiyo itasaidia kuweka nchi zetu katika hali nzuri kiuchumi" Alisema

Kwa upande wake Muandaaji wa Warsha hiyo kutoka chuo cha MS TCDC Makena Muthuri amesema wameshukuru sana kwa ujio wa Waziri Mkuu katika warsha hiyo na kwamba lengo ni kuwakutanisha vijana pamoja kubadilishana uzoefu lakini pia kutumia fursa zilizopo katika kukuza uchumi.

Ameongeza kuwa Warsha hiyo itaendelea kwa siku tano mfululizo ili kukaa kwenye vikundi  na kuja na mawazo yatakayo jenga nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela katika uzinduzi wa jukwaa la vijana YouLead, Mkoani Arusha. Kushoto ni katibu Mkuu wa Jumuiya Afrika Mashariki Peter Mathuki (Picha na Jane Edward, Arusha)

Mkurugenzi mtendaji chuo cha MS TCDC Bi Makena Muthuri, akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Warsha ya vijana (YouLead)picha na Jane Edward, Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...