Na Humphrey Shao, Morogoro
WAZIRI wa Maji Juma Aweso ameanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji na mito ambayo imechepushwa huku akitoa maelekezo ya kutaka kuwe kunafanyika operesheni endelevu kukagua.
Katika ziara hiyo Waziri Aweso ameongizana na Mkurungezi wa Bonde la Wami Ruvu,Mtendaji Mkuu wa Dawasa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Baada ya kukagua maeneo yenye vyanzo vya maji pamoja na uchepushaji wa mito Aweso ametoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro na Mkurungezi wa Bonde la Wami Ruvu kuhakikisha wanafanya operesheni hizo endelevu kudhibiti uvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji.
"Mnatakiwa kuwa na mpango mkakati na endelevu wa kudhibiti uharibifu wa mazingira na unyweshaji wa mifugo katika mto kwa kuunda Task force kuanzia ngazi ya kijiji,"amesema Aweso.
Ameongeza kwamba lazima Serikali za vijiji vishirikishwe katika mpango wa kulinda maeneo hayo kwani zina mamlaka kamili na sio serikali tegemezi.Ametaja kuwa ameshuhudia kundi kubwa la mifugo eneo la Dutumi pamoja na wakulima kuechepusha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando Amesema wao kama sehemu ya kamati ya ulinzi na usalama wamepokea maelekezo ya Waziri na watayafanyia kazi.
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso(Mb) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja na watumishi wa Bonde la Wami Ruvu katika utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuondosha watumiaji wasio rasmi katika mto Ruvu ambao kina chake kimepungua kutokana na ukame.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...